Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Uhusianao wa Wakala wa Uchimbaji Visima na
Mabawa (DDCA) Bw. Nungu Egwagwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu miradi iliyokwisha tekelezwa na wakala huo tangu
kuanzishwa kwake ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa maji yenye ujazo wa
mita zaidi ya milioni 23,000 kutokana na uchimbaji wa visima na
Mabwawa.Kushoto ni Afisa Masoko na Uhusiano Bi. Ashura Katuga kutoka
wakala huo.
…………………………………………………………………………………………………..
Frank Mvungi-Maelezo
Wakala wa Uchimbaji visima na
Mabwawa (DDCA) Umewezesha kupatikana kwa maji yenye ujazo wa mita zaidi
ya milioni 23,000 kutokana na uchimbaji wa visima na mabwawa
uliofanywa na wakala huo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es salaam na Mkuu wa kitengo cha masoko na Uhusianao wa wakala huo
Bw. Nungu Egwagwa wakati akitoa taarifa kuhusu miradi iliyokwisha
tekelezwa na wakala huo tangu kuanzishwa kwake.
Akifafanua Egwagwa amesema kuwa
lengo la wakala huo ni kusaidia kutatua tatizo la upatikanaji wa maji
kwa kuchimba visima na mabwawa kwa gharama nafuu ambazo wananchi walio
wengi wanamudu.
“Tunachokifanya ni kutoa huduma
zaidi kuliko kufanya biashara kama Taasisi ya Serikali tukiwa na dhamira
ya kusaidia wananchi kuwa na visima na mabwawa yenye ubora
unaotakiwa”.Alisisitiza Egwaga
Akizungumzia miradi
iliyotekelezwa na Wakala huo, Egwaga amesema kuwa mpaka sasa Wakala
umekwishajenga mabwawa 23 katika kipindi cha januari 1997 hadi june,2016
katika mikoa mbamimbali ikiwemo Tanga,Shinyanga, Tabora, Mtwara
naPwani.
Akitaja mikoa mingine ambako mabwawa hayo yamejengwa Egwaga alisema kuwa ni Ruvuma,Manyara,Mbeya, mwanza, Lindi na Mara.
Akitoa mfano wa miradi ya
uchimbaji visima Egwaga alisema kuwa moja ya miradi iliyotekelezwa ni
ule wa kuchimba visima katika chuo Kikuu cha Dodoma hali iliyosaidia
kuondoa kabisa tatizo la maji katika chuo hicho na katikamanispaa ya
Dodoma.
Pia Egwaga alitoa wito kwa
watanzania kutumia huduma zinazotolewa na wakala huo ikiwemo kufanya
utafiti wa maeneo yanayofaa kuchimba visima virefu,kujenga malambo na
mabwawa,kupima wingi na ubora wa maji yatokayo kwenye visima na ujenzi
wa miradi midogomidogo ya mifumo ya usambazaji maji.
Madhumuni ya DDCA ni kuongeza
kasi ya kutafuta na kuviendeleza vyanzo vya maji kwa gharama nafuu ili
kuboresha huduma ya upatikanaji maji safai na salama na kutosha kwa
matumizi mbalimbali yakiwemo ya majumbani,mashambani,mifugo,ufugaji
samaki na viwandani.
0 maoni:
Chapisha Maoni