Mripuko
mkubwa umetokea katika mji wa Medina nchini Saudi Arabia.shuhuda wa
tukio hilo anaeleza kwamba mtu aliyejitoa muhanga alifyatua kitufe cha
kujilipulia karibu na msikiti mkubwa wa mtume, ambapo msikiti huo ni
mmoja wapo ya eneo takatifu kwa waislamu.
Kituo
cha runinga mjini Saudia kilionesha picha za moto mkubwa uliokuwa
ukiwaka kwenye maegesho ya magari huku magari yakiteketea na mwili mmoja
wa binaadamu ulionekana karibu yake.
Mpaka
sasa hakuna kauli yoyote iliyotolewa na serikali ya Saudi Arabia
kuhusiana na tukio hilo.tukio hili limetokea huku mtu mwingine wa
kujitoa muhanga akiwa amejiripua katika msikiti wa madhehebu ya Shia
upande wa Mashariki mwa mji wa Qatif, na mripuko wa tatu umetokea karibu
na ubalozi wa Marekani mjini Jeddah.
Askari
wawili wa kulinda usalama wamejeruhiwa katika mojawapo ya matukio
hayo.na hakuna taarifa zozote kuhusiana na kundi lililo husika kupanga
na kutekeleza mashambulizi hayo kuwa ni akina nani.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni