Mkuu
wa Wilaya ya Mpwawa iliyopo mkoani Dodoma, Mohamed Utaly (wa pili
kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo asubuhi, kuhusu harambee ya kupata fedha za kununulia
madawati itakayofanyika Juni 4 mwaka huu Ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald
Ngwenzi,Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje na Mkuu wa Kitengo
cha Manunuzi, Samuel Albertus Coy.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia
ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Utaly.Na Dotto Mwaibale
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpwapwa Dodoma
Juni 4 mwaka huu inatarajia kufanya harambe ya kupata fedha za kununulia
madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari wilayani humo ambayo
itafanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu wa Wilaya hiyo
Mohamed Utaly alisema wamefikia hatua hiyo ili kukabiliana na uhaba wa
madawati katika shule hizo ambapo pamekuwa na changamoto kubwa.
Alisema awali halmashauri hiyo ilikuwa
na upungufu wa madawati 16,000 lakini baada ya kuwashirikisha wananchi
na kufanya harambee mbalimbali walifanikiwa kupata madawati 6000 na
kubaki kiasi cha madawati 10,000 ambayo yanahitaji.
Utaly alisema halmshauri hiyo katika
bajeti yake ya mwaka 2015-2016 ilitenga sh. milioni 180 kwa ajili ya
madawati ambapo kunamafanikio makubwa ya kupata madawati hayo
yaliyosalia hivyo akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa ndani
wa wilaya hiyo na nje kujitokeza katika harambee hiyo ili waweze
kufanikisha jambo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo
Mohamed Maje alisema changamoto kubwa waliyoibaini ni kutokuwa na
kitengo cha kufanya ukarabati wa madawati yaliyo haribika ambacho hivi
sasa kimeanzishwa.
"Kwa muda mrefu hatukuwa na kitengo cha
kukarabati madawati yaliyoharibika lakini sasa tumekianzisha na
kitasaidia kupunguza changamoto hiyo kwa kitengo hicho kitakuwa
kikisaidia na wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya watu 20 ambavyo
vipo sita kwa ajili ya kufanya kazi hiyo" alisema Maje.
0 maoni:
Chapisha Maoni