…………………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Umma nchini waliopewa dhamana
serikalini kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuepuka
malalamiko yasiyo ya lazima kwa wanaowahudumia.
Waziri Kairuki aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2016 mkoani Singida.
“Najua miongoni mwa watumishi wa
umma wapo watumishi waliopewa dhamana lakini utoaji wao wahuduma
unatiliwa shaka. Hawapendi kusikiliza matatizo ya wateja wa ndani yaani
watumishi wenzao,” Mhe. Kairuki alisema.
Amewataka watumishi wenye tabia
hizo kuacha mara moja na kuishi maisha ya kazi kama Mkataba wa Huduma
kwa Mteja unavyowaongoza katika kutoa huduma kwa kiwango kwa wateja wote
wa ndani na nje ya taasisi.
Aidha, Mhe. Kairuki amewataka
Watendaji kutenga muda wa kukaa na watumishi wao ili kusikiliza kero na
changamoto zinazowakabili kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.
“Uzoefu unaonyesha kuwa watumishi
wanaposhirikishwa katika masuala yanayowagusa kama tulivyo hapa basi
huduma kwa wananchi na wadau wengine zitaboreka na kazi kufanyika kwa
ari na hivyo kuongeza tija na ufanisi kazini,” Waziri Kairuki aliongeza.
Katika hatua nyingine, Mhe.
Kairuki alifanya ziara katika Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Singida
na kuzungumza na watumishi wa chuo hicho ambapo aliwataka watumishi hao
kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuwajibika ili kuleta
matokeo bora kwa taifa.
“Tuwewabunifu,
tuangalievipaumbele, tufundishe kozi ambazo hazifundishwi sehemu
nyingine ili kuweza kupata soko zuri zaidi,” Waziri Kairuki alisisitiza.
Aliwasisitiza watumishi hao kuwa
na ushirikiano na vyuo mbalimbali hasa katika nyanja za utafiti, mafunzo
na masuala mengine ya maendeleo ili kuboresha chuo hicho.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi
wa Umma ambayo hufanyika kuanzia tarehe 16-23 Juni, kila mwaka, kwa
mwaka 2016 yanafanyika kwa namna tofautia mbapo Viongozi na Watendaji
wanakutana na wateja wao wa ndani na nje ya taasisi zao kwa lengo na
kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika kutekeleza hilo, Mhe.
Kairuki amezindua maadhimisho hayo kwakufanya vikao kazi na watumishi wa
mkoa wa Singida kutoka katika kada mbalimbali za utumishi wa umma.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika kwa mwaka 2016 ni “Uongozi wa Umma kwa ukuajiJumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka.”
Kaulimbiu hiyo inaambatana na kaulimbiu ndogo ambazo ni: Mchango wa Utumishi wa Umma katika Ukuaji wa Uchumi Barani Afrika na Mchango
wa Utumishi wa Umma katika Kuiwezesha Ajenda ya Afrika ya 2063 ambayo
inaweka mkazo katika Maendeleo ya Afrika na Haki za Wanawake.






0 maoni:
Chapisha Maoni