Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Prof. Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
KITUO
cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for
Agricultural and Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya
(EU) chenye makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais
Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador)
wa Maendeleo ya Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pacific.
Katika barua iliyokabidhiwa na
mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk.
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameteuliwa kwa kutambua
mchango na juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na
barani Afrika.
Katika wadhifa wake huo mpya, CTA
imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha katika makongamano ya
kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa kukiendeleza kilimo kwa ajili
ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na uhakika kwa vijana na wanawake
katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA
katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika
nchi mbalimbali.
Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo
na kuahidi kushirikiana na CTA katika kutekeleza mambo ambayo ameombwa
kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya
na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki wenye makao makuu
mjini Brussels, Ubelgiji.
Prof. Kamuzora ambaye pia ni
Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya CTA akiwakilisha nchi za
ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano tangu 2013 hadi 2018
0 maoni:
Chapisha Maoni