Wapiganaji
tisa wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Libya wameuawa na
wengine 50 kujeruhiwa katika makabiliano ya kusambaratisha kundi la
Islamic state kutoka kwa ngome yake ya Sirte, msemaji wa hospitali
amesema, nashirika la habari la Associated Press kuripoti.
Wapinganaji
hao walifariki kutokana na mashambulio ya bunduki zilizowalenga moja
kwa moja, ama kwa mashambulio ya mabomu yaliyotegwa barabarani katika
vita vya mapema wiki hii.
Sirte ni
eneo ambalo aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alizaliwa kabla
ya kuuawa na jeshi la muungano wa NATO mwaka 2011.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni