Katika
kuhakikisha wafanyakazi wake wanapata elimu ya masuala mbalimbali ya
kijamii nje ya mazingira ya kazi,kampuni ya TBL Group imewezesha baadhi
ya wafanyakazi wake kuhudhuria semina ya malezi ya familia iliyofanyika
jijini Dar es Salaam .
Katika
semina hiyo wataalamu mbalimbali wa masuala ya elimu jamii kutoka
kampuni ya Grace Inc walitoa mada kuhusiana na masuala ya malezi bora ya
familia na changamoto zilizopo katika kujenga familia bora ambapo
washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali yanaohusiana na malezi ya
familia.
Wafanyakazi
hao walishukuru kampuni kwa kuwapatia fursa ya kuhudhuria semina hiyo
na walisema kuwa imewawezesha kupata maarifa mbalimbali yatakayowasaidia
kujenga familia zao.
Watoa
mada Grace Makani Tarimo na Dk.Ellivid Waminian wakiongea na washiriki
wa semina ya masuala ya kujenga familia bora iliyofanyika katika hoteli
ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wakisikiliza mada.
Wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika semina.
0 maoni:
Chapisha Maoni