Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibhundughulu Halmashauri
ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya ambao ndio watumiaji wa daraja hilo la
Mbaka ambalo lilikwama kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha hali
iliyopelekea wananchi wa kuanza kutumia daraja hilo kwa kupita juu kwa
kutumia kamba hali ambayo iliatalisha maisha yao.
Katika
mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuwapa
ushirikiano mafundi wanaojenga daraja hilo ili liweze kukamilika kwa
wakati .
Aidha
Makalla amekemea baadhi watu wasio waaminifu ambao walikuwa wakipita
juu ya daraja hilo kabla ya kukamilika kwakwe kitendo ambacho
kilikuwahatari kwa maisha ya wananchi hao.
Aidha
amemtaka mkarandasi anaye jenga daraja hilo kuhakikisha anakamilisha
ujenzi huo katika kipindi cha wiki mbili ili kutoa fursa kwa wananchi
hao kuanza kulitumia .
|
0 maoni:
Chapisha Maoni