Jumamosi, 25 Juni 2016

Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe afungua mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango

SONY DSC
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango unaofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma. Alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mge. Dkt. Philip Mpango. Kaulimbiu ya Mkutano ni Kuelekea kwenye Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21.
k2 Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kufungua mkutano huo. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
SONY DSCKaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri akizungumza katika mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango unaofanyika mjini Dodoma.
k4Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
unspecified Washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Wachumi na Maafisa Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto waliokaa mwenye miwani).
Picha na mpiga picha wetu

0 maoni:

Chapisha Maoni