Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli akikabidhi tuzo
kwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora wa mwaka 2015,
kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin wakati wa hafla ya
kutoa tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda
Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia) na kushoto ni
Waziri wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Rais
John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha
wafanyabiashara wenye viwanda na watendaji wa makampuni ambayo
yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka huu
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo
waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo.
…………………………………………………………………………………………………………………
Kampuni ya TBL Group imeibuka
mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha
mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la
uzalishaji wa vinywaji ambapo imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla
ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es
salaam katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa
heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni
zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni kwa kuwa jitihada za kila mmoja
ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha
kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu
ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu
unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali
zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea
kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa
ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira
nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa
wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya
kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa
kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa
karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza
kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.
Kampuni ya TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya
Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka
mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo
imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla
ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es
salaam katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa
heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL
Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote
wa kampuni kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio
haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi
tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na
tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea
kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi
mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini
na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za
serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa
ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana
nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari
imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa
bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa
karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza
kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.
0 maoni:
Chapisha Maoni