Rais wa
Marekani, Barack Obama, ameshtumu vikali matamshi ya mgombea urais kwa
tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwamba waislamu
wasiruhusiwe kuingia Marekani. Obama amesema hiyo 'si marekani
wanayohitaji.'
''Kuwabagua
Waislamu wa Marekani kutasababisha nchi hiyo kukosa usalama,na kuongeza
tofauti iliopo kati ya nchi za magharibi na zile za kislamu'', Obama
alisema
Siku ya
Jumatatu bwana Trump, aliongezea kuhusu mpango wa kupiga marufuku nchi
zote ambazo zina historia ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Marekani.
Alisema shambulio la ufyatuliaji risasi la Orlando linathibitisha yote.
Watu 49
waliuawa, baada ya Omar Mateen raia wa Marekani ambaye wazazi wake ni
raia wa Afghan kufyatua risasi katika kilabu ya wapenzi wa jinsia moja
huko Orlando.
Bwana Trump
amesema pendekezo lake litatekelezwa kupitia (uamuzi wa pamoja ) iwapo
rais atapewa mamlaka ya kupiga marufuku uingizaji wa watu wenye daraja
lolote katika nchi hiyo jambo ambalo rais ataliona kuleta madhara ya
kiusalama kwa Marekani.
0 maoni:
Chapisha Maoni