Mkutano
wa nganzi ya juu kuhusu Ukimwi jana ( Alhamis) uliingia katika siku
yake ya pili ambapo viongozi mbalimbali wakiwamo Mawaziri na Naibu
waziri wanaohusika na masuala ya afya wameendelea kuelezea nini ambacho
nchi zao zinatekeleza katika kukabili na kudhibiti maambukizi mapya ya
Virusi vinavyo sababisha Ukimwi pamoja na huduma wanazopatiwa watu ambao
wamekwisha kuathirika na kuugua.
Mmoja
ya nchi ambayo iliwasilisha mafanikio, changamoto na mwelekeo wa
baadaye katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa Ukimwi, ugonjwa ambao
Jumuiya ya Kimataifa umejiweka lengo la kuutokomeza ifikapo mwaka 2030
ili kuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Juhudi
za Tanzania dhidi ya Ukimwi, zilielezwa na Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dr. Hamis A Kigwangalla
(Mb). Ambaye katika maelelezo yake, amesema, Tanzania inaamini kuwa
inawezekana kufikia hali ya kutokuwa na maambukizi mapya, kumaliza
ubaguzi na unyanyapaa, na kuwa na kiwago sifuri cha vifo vinavyohusiana
na Ukimwi fikapo mwaka 2030.
Hata
hivyo anasema, ili kufikia hatua hiyo au mafanikio hayo, mambo kadhaa
yanapashwa kufanyika, yakiwamo ya uimarishwaji wa elimu ya kinga, vijana
na jumuiya kwa ujumla kufundishwa mbinu za kuepukana na tabia hatarishi
ambazo zinachangia ongozeko la waathirika na kuhakikisha upatikanaji
kirahisi wa za dawa na ambazo zitakuwa za gharama nafuu.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika
mkutano huu, amekwenda mbali zaidi kwa kusema pia patahitajika kupunguza
vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watu wanaoishi na Virusi
vya Ukimwi, kujadili masuala ya jinsia pamoja na mila na tamaduni,
kutenga raslimali za kutosha kwaajili ya watu wenye mahitaji wakiwamo
vijana, kuwa na viwanda vitakavyoweza kuzalisha dawa.
Akizungumza
baadhi ya mafanikio ambayo Tanzania imekwisha kuyafikia katika kukabili
tatizo la Ukimwi, Naibu Waziri ameyataja baadhi ya mafanikio hayo kuwa
ni pamoja na kupunguza maambukizi mapya kutoka 140,000 mwaka 1990 hadi
kufikia 63,000 mwaka 2014. Vile vile vifo vitokanavyo au
vinavyosaabishwa na ukimwi pia vimepungua kwa asilimi 40 katika kipindi
hicho.
Akaeleza
pia kwamba hata watu wanaopatiwa huduma ya matibabu nayo imeongezeka
kufikia asilimia 60 huku ongezeko likiwa kwa watoto na hasa baada ya
kupitisha mpango unaotambulika kama Option B+ miaka sita iliyopita.
Kuhusu
kupungua kwa raslimali fedha hususani kutoka kwa wafadhili, Dr.
Kingwangalla, amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo, na kwa
kuzingatia wito wa jumuiya ya kimataifa kupanua wigo wa mapato ya ndani,
serikali ya Tanzania ilianzisha Mfuko wa ukimwi, (AIDS Trust Fund)
mfuko anaosema hadi sasa serikali ndiyo imekuwa mchangiaji mkuu, ingawa
pia kwamba sekta binafsi nayo inatazamiwa kuchangia.
Akasema
sehemu au nusu ya fedha hizo (55%) itakwenda kusaidia upatikanaji wa
huduma na kuongeza kuwa juhudi hizo za serikali pia zimesaidiwa na
ushirikiano baina ya Tanzania na nchi nyingine rafiki pamoja na
mashirika ya kimataifa na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wale wote
ambao wanachangia juhudi za serikali.
Kuhusu
mipango mingine ambayo serikali inaendelea nayo , Naibu waziri alikuwa
na haya ya kueleza “ baada ya kuwa tumeanza utaratibu wa kupima na
kutibu kwa baadhi ya wilaya chache nchini, tunakusudia kuisambaza huduma
hiyo lakini itakuwa ni kwa hatua ili kutoa nafasi ya kuwajengea uwezo
watoaji wa huduma ya afya, kuhuisha mifumo ya usambazaji wa vifaa ikiwa
ni pamoja ushiriki wa jamii ili iweze kupokea na kuukubali mfumo huu
mpya wa utoaji wa huduma” ameeleza Naibu Waziri.
Akasisitiza
zaidi kwa kusema ingawa ugonjwa wa Ukimwi umeendelea kuwa changamoto
kubwa kwa maendeleo ya nchi ambapo inakadiriwa watu 1.5 milioni
wameathirika, huku mzingo mkubwa ukiwaelemea wanawake na vijana hasa
watoto wa kike, serikali ya tanzania itaendelea na jitihada zake za
kuhakikisha inafikia lengo la kutokuwa na maambukizi mapya, kutokomeza
unyanyapaa na ubaguzi, na vifo vinatokanavyo na ukimwi.
Katika
hatua nyingine amesema ili kutorudisha nyuma mafanikio ambayo Tanzania
imeyafikia hadi sasa pamoja na nchi nyingine kusini mwa Jangwa la Sahara
Jumuiya ya Kimataifa inaombwa kusaidia jitihada zinazofanywa na
serikali za nchi hizo za kuwa na mapato yake yenyewe ya kugharamia
huduma za afya kwa wagonjwa wa ukimwi na pamoja na huduma nyinginezo
badala ya kuziachia kabisa jukumu hilo.
Na Mwandishi Maalum, New York
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dr.
Hamisi Kigwangalla ( Mb) akizungumza kwa niaba ya Serikali kuhusu
mafanikio na changamoto ambazo serikali imekuwa ikikabiliana nazo dhidi
ya ugonjwa wa UKIMWI ni katika mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa kuhusu ukimwi unaoendelea hapa Umoja wa Mataifa, Naibu
Waziri anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu.
Naibu
Waziri Mhe. Dr. Hamisi Kingwangalla akiwa katika picha ya pamoja mbele
ya bendera ya Tanzania na sehemu ya ujumbe wa Tanzania unaoshiriki
mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Ukimwi, mara tu baada ya kusoma hotuba
yake katika Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo mkutano
huu wa siku unafanyika.
0 maoni:
Chapisha Maoni