Ongezeko
la idadi hiyoinafanya Mkoa wa Iringa kuwa na jumla ya watumishi hewa 197 baada
ya taarifa za awali kueleza uwepowa watumishi 27 hewa mkoani hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana mkuu wa mkoa wa Iringa
Amina Masenza alisema watumishi hao wamegawanyika katika makundi matatu ambayo
ni kundi la wasitaafu,watoro na waliofarikiambao waliendelea kulipwa mishahara.
“Mtakumbuka
kuwa April 18 mwaka huu nilitoa taarifa
ya idadi ya wafanyakazi hewa 21 lakini nikaeleza kuwa ninaunda timu ya wataalam
kuchunguza jambo hili ili kujiridhisha na
kuondokana kabisa na tatizo la watumishi hewa mkoani hapa”alisema Masenza na kuongeza:
“Timu
niliyounda imemaliza kazi na kunikabidhi
ripoti Juni 7 mwaka huu ,kwa ufupi ni
kwamba timu imegundua uwepo wa wafanyakazi hewa 169 katika halmashauri zote
tano za mkoani hapa,pia watumishi hao wameisababishia serikali hasara ya Sh 364,028,910.80”alisema.
Sambamba
na watumishi hewa Mkuu huyo wa mkoa alibainisha tatizo lingine lililoibuliwa na
timu yake ya wataalamu kuwa ni suala la matumizi
mabaya ya fedha zaserikali yaliyofanywa na uongozi wa hosptaliya Teuli ya Ilula
inayotoa huduma katika Wilaya ya Kilolo.
Alisema
timu hiyo libaini matumizimabaya ya Sh
151,583,969.00 ambalo alidai lilikuwa la mishara isyolipwa na hazikurejeshwa
hazina tangu mwaka 2008 hadi februari 2016..
“Fedha
hizo ambazo kisheria ilibidi zirejeshwa hazina zilitumika kugharamia shughuli
za uendeshaji wa hosptali hiyo ikiwamo kulipa mishara watumishi ambao orodha
yao haijajuloikana serikalini,kununu dawa na kulipiagharama za umeme pasipo idhini ya serikali”alisema Masenza.
Masenza
alisema serikali inaendeela na uchunguzi dhidi ya jambo hio na hatua
zitachukuliwa ikwia ni pamoja na
kufanyia kazimapendekezoya ripoti ya wataalamu.
Akizunguzia
suala la watumishi hewa serikali imejipanga
kuchukua hatua dhidi ya watumishi wote waliohusika na kusababishia uwepo wa
watumishi hewa waliosababuishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Akizungumzia
suala hilo mkazi wa Iringa Ramadhan Mahano alipongeza serikali ya mkoa kuweza
kubainisha watumishi hewa na kuishauri kulifanya jambohilo kuwa la kudumu ili
kulifanya tatizo
lawatumishihewakutojirudia.
“Wanaochangia
uwepo wa watumishi hewa ni watumishi pia niombe serikali ifafanya uchunguzi wa
kina na wahusika wote wafikishwa mahakamani ili haki iweze kutendeka,
kwakufanya hivyo kutasaidia kuondoa tatizo hilo kabisa”alisema Mahano.
Katika
hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa alisema
bidhaa ya sukarimkoani hapaimeadimika na kwamba kampuni ya Mohamed Intrepraise
LT D inatarajia kuingiza sukarihiyokuanzia leo.
“Sukaria
imeadimika na imepanda bei kutoka Sh 1800 ya zamani hadikufikia 2800 na3000,Iringa hatuna kiwanda cha sukari na
sukariinayotumika hapani kutoka nje ya mkoa wa Iringa,kwa sasa msihofu
serikaliyenuimechukuahatua ya kuyaomba makampuni makubwa kuleta sukari kuanzie (kesho)
leo”alisema Masenza.
0 maoni:
Chapisha Maoni