Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Happiness Mgalula akitoa hotuba wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi
na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma mjini
Dodoma, Kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo, dkt. John Mduma kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji,
Klasta ya Uchumi Jumla kutoka Tume ya Mipango dkt. Lorah Madete.
Washiriki katika hali ya utulivu wakati wa mafunzo katka ukumbi wa Chuo Cha VETA mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia mafunzo,
wanaoonekana mbele, kulia ni Dkt Lorah Madete (aliyevaa nguo za rangi ya
bluu) na kushoto ni Bibi Angela Shayo (mwenye koti jeusi), wote
(wawili) kutoka Tume ya Mipango.
Washiriki katika hali ya utulivu wakati wa mafunzo katka ukumbi wa Chuo Cha VETA mjini Dodoma.
Washiriki wakifuatilia wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) moja ya mada katika mafunzo ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma.
Washiriki katika hali ya utulivu wakati wa mafunzo katka ukumbi wa Chuo Cha VETA mjini Dodoma.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya Usimamizi
na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Umma kanda ya
kati inayojumuisha mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma.
Na Adili Mhina, Dodoma.
Tume ya Mipango imewashauri
maofisa wa serikali wenye dhamana ya kusimamia miradi ya umma
kuhakikisha wanatumia mbinu za kisasa katika kuchambua, kuchagua,
kutekeleza na kusimamia miradi ya serikali ili kuhakikisha malengo ya
Dira ya Taifa ya Maendeleo yanafikiwa kwa wakati.
Ushauri huo umetolewa jana mjini
Dodoma na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta
ya Miundombinu na Huduma, Mhandisi Happiness Mgalula alipokutana na
maofisa mipango wa Ofisi za Mikoa na Halmashauri za kanda ya kati
iliyojumuisha Mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara kwa lengo la kutoa
elimu katika kuandaa, kusimamia, na kutekeleza miradi ya Umma.
Alisema kuwa Serikali ilifanya
tathmini na kugundua kuwa hakuna vigezo vinavyofanana katika kuandaa na
kuchagua miradi ya umma katika taasisi mbalimbali za Serikali kitu
kinachorudisha nyuma juhudi za kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025.
“Dira ya Taifa ya Maendeleo
inaelekeza kuwa hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania inatakiwa iwe inchi ya
uchumi wa kati na kwa vile tumedhamiria kwa dhati kifikia hapo ni lazima
tujipange upya na kutumia utaalamu wa kisasa na vigezo vinavyofanana
katika kuchagua miradi yenye uwezo wa kulifikisha taifa huko,” alisema
Mgalula.
Kukosekana kwa vigezo
vinavyofanana kumesababisha upungufu mkubwa katika miradi ya umma huku
ikipelekea miradi mingine kukosa mikopo katika soko la mitaji la ndani
au la kimataifa kutokana na kuwa na maandiko yasiyokidhi vigezo
vinavyohitajika.
Mgalula aliongeza kuwa ili
kuwekeza katika miradi yenye tija itakayoharakisha Tanzania kuingia
katika nchi za uchumi wa kati, Tume ya Mipango imedhamiria kuendelea na
utaratibu wa kutoa mafunzo kwa walengwa nchi nzima ili kuongeza utaalam
katika kuweka vipaumbele vichache vyenye ufanisi kwa kila mwaka wa
bajeti kuliko kuwa na miradi mingi isiyokamilika.
Na kwa upande wa maafisa wanaopata
elimu hiyo wanakiri kuwepo kwa changamoto nyingi katika maandalizi ya
miradi ya umma kutokana kukosekana kwa mfumo unaofanana katika uwekezaji
wa miradi ya umma.
“Tayari tumeanza kuelekezwa namna
ya kuandaa miradi kwa kuzingatia vigezo vya kisasa viliyoainishwa katika
mwongozo wa usimamizi wa uwekezaji wa miradi ya serikali, hii
itatusaidia kuwa na utaratibu mmoja na unaoeleweka tofauti na
ilivyokuwa zamani ambapo kila mradi mpya ulikuwa na mfumo wake” Alisema
Bwana Mkama kutoka Dodoma.
Naye Afisa Mipango kutoka
Halmashauri ya Babati Bw. Godlisten Geofray alieleza kuwa kuwepo kwa
mfumo wa kisasa kutasaidia kuweka kumbukumbu sahihi za miradi hata ile
ambayo haitafanikiwa kupata fedha kwa mwaka husika pale mfumo wa
kanzidata utakapoanzishwa ambao utahifadhi kubukumbu za miradi yote
nchini.
Washiriki wa mafunzo hayo
wameonesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Tume ya Mipango katika
kutoa elimu hiyo katika ngazi mbalimbali huku wakieleza kuwa utaratibu
huo utasaidia kuimarisha mawasiliano kwenye bajeti ya miradi kati ya
serikali kuu na serikali za mitaa.
Wataalamu hao wamesisitiziwa kuwa
miradi yote itakayohitaji fedha za Serikali katika Bajeti italazimu
kufuata utaratibu uliobainishwa katika Mwongozo wa Usimamizi na
Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma ili kuweza
kuimarisha ufanisi na kupata thamani ya fedha.
0 maoni:
Chapisha Maoni