Posted by Esta Malibiche on Sept10.2016 in News
Mkuu wa wilaya Bariadi mkoani Simiyu Festo Kiswaga amewataka
wananchi wilayani humo kujitokeza kwa wingi katika kilele cha mbio za mwenge wa uhuru kitaifa zinazotarajiwa
kufanyika mwezi October 14.2016 wilayani humo.
Kiswaga alisema kuwa sherehe hizo zitakazoambatana na
kumbukumbu ya baba wa Taifa na kilele cha wiki ya vijana Duniani.
Akizungumza na wananchi wa bariadi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
jana katika eneo la stendi ya zamani na kukagua na barabara eneo linalojengwa karavati ikiwa ni moja ya maandalizi.
‘’’Ninawaomba wananchi wa wilaya ya Bariadi tujiandae kupokea ugeni mkubwa kutoka nje ya mkoa,ugeni
wa kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha sherehe zinafana na kufanyika kwa Amani
na utulivu’’’’’alisema Kiswaga
Alisema Mwenge wa uhuru wilayani humo,unatarajia kuwasili
October 12,ambapo utakimbizwa bariadi
mjini, October 13 utakimbizwa Halmashauri ya Bariadi na October 14 kilele cha mbio za
mwenge kitaifa zitakazofanyika Bariadi Mjini ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa
Rais wa awamu ya tano Dkt.John Pombe Magufuli.
Wananchi wa bariadi wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya hiyo katika mkutano uliofanyika jana |
0 maoni:
Chapisha Maoni