![]() | |
|
SERIKALI
kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imefafanua kuwa Washirika wa
Maendeleo bado wanaendelea kuisadia katika bajeti yake na kwamba tuhuma
za kujitoa kwa makundi 14 ya kuisaidia bajeti sio za kweli.
Imesisitiza
kuwa bado makundi hayo yanaendelea kuisaidia bajeti ya Tanzania, na kwa
mwaka wa fedha 2015/2016, Washirika wa Maendeleo wanane waliahidi
kuendelea kusaidia Bajeti Kuu wakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika,
Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ireland, Sweden na Benki ya
Dunia.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius
Likwelile, kwa mwaka wa fedha 2016/2017 baadhi ya Washirika wa Maendeleo
wameshathibitisha kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali. Aliwataja kuwa ni
pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Denmark, Umoja wa Ulaya pamoja
na Benki ya Dunia.
Wengine
watakaoendelea kuisaidia Serikali kupitia wa Mfuko wa Pamoja wa
Maendeleo na Miradi. Hao ni pamoja na Ubelgiji, Canada, China, Denmark,
Finland, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, India, Italia, Japan, Korea
Kusini, Norway, Sweden, Uholanzi, Uingereza, Marekani na Uswisi.
Washirika
wengine wa maendeleo ambao wanaisaidia bajeti ya Serikali ni Benki ya
Maendeleo ya Afrika, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, BADEA, Mfuko wa OPEC
pamoja na Saudi Arabia, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.
Taarifa
hiyo ya Dk Likwelile iliongeza kuwa Serikali ya pamoja na Washirika wa
Maendeleo wanaoisaidia Tanzania wako katika mazungumzo juu ya namna ya
kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hizo.
“Serikali
imewashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea kuisaidia Tanzania
katika kupelekea juhudi za kimaendeleo zenye tija kwa wananchi,” alisema
Dk Likwelile.







0 maoni:
Chapisha Maoni