Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Yombo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani, Salimu Juma
Mavaga (kushoto), akizungumza wakati wa kupokea vizimbuzi ‘ving’amuzi’
vya Kampuni ya StarTimes vilivyo tolewa kwa gharama ya sh,50,000 kwa
wananchi wa vijiji vitatu vya Yombo, Chasimba na Maimbwa wilayani humo
jana.
Bibi
Maendeleo ya Ustawi wa Jamii wa Kata hiyo, Melitha Kiwanga akizungumza
katika mkutano huo wakati akiishukuru kampuni ya StarTimes kuwapelekea
vizimbuzi hivyo.
Meneja
Mauzo wa StarTimes, Tanzania, Tang Jing Yu akizungumza katika mkutano
huo kuhusu ugawaji wa vizimbuzi hivyo na nia ya Rais wa China ya
kusaidia nchi za Afrika katika mfumo wa mawasiliano wa Kidigitali.
Meneja
Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing (kushoto), akizungumza katika mkutano
huo. Kulia ni Ofisa wa Idara ya Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Mayala.
Mgeni
rasmi katika shughuli hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashidi Kiwamba,
akizungumza kwenye mkutano huo wakati akiishukuru kampuni hiyo kwa
kuwapelekea vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wakisubiri kulipia vizimbuzi hivyo na kwenda kufungiwa.
Wakina mama wakisubiri kulipia vizimbuzi hivyo.
Mgeni
rasmi katika shughuli hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashidi Kiwamba
(kushoto), akimshukuru Meneja Mauzo wa StarTimes, Tang Jing Yu kwa
kuwapelekea huduma hiyo ya vizimbuzi katika karafa yao.
Mwalimu Hilda Stambuli wa Shule ya Msingi ya Yombo akishukuru kwa niaba ya wenzake kwa kupelekewa vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu.
Meneja
Mauzo wa StarTimes Tanzania, Tang Jing Yu (wa tatu kushoto),
akimkabidhi Mkazi wa Kijiji cha Matimbwa, Shaabud Abdallah (wa pili
kulia), Kizimbuzi na Dishi lake baada ya kulipia sh.50,000 katika hafla
iliyofanyika Kata ya Yombo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani jana. Wengine
wanaoshuhudia kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing,
Ofisa Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Yombo,
Salimu Juma Mavaga na Fundi Mkuu wa StarTimes Michael Mkufya.
Ofisa
Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba (katikati), akimkabidhi Kizimbuzi Mkazi
wa Kata ya Yombo, Ramadhan Kibwana Shomari (wa pili kulia), baada ya
kukilipia. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes,
Furaha Mayala, Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Mtendaji
wa Kata ya Yombo, Salimu Mavaga, Meneja Mauzo Tang Jing Yu na Fundi Mkuu
wa StarTimes, Michael Mkufya.
Ofisa
Tarafa ya Yombo, Rashid Kiwamba (katikati), akimkabidhi Kizimbuzi Mkazi
wa Kijiji cha Chasimba,Miraj Mukadase (wa pili kulia), baada ya
kukilipia. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Idara ya Masoko wa StarTimes,
Furaha Mayala, Meneja Mauzo wa StarTimes, Yan Jing Jing, Ofisa Mtendaji
wa Kata ya Yombo, Salimu Mavaga, Meneja Mauzo Tang Jing Yu na Fundi Mkuu
wa StarTimes, Michael Mkufya.
Mkazi wa Kijiji cha Matimbwa, Shaabud Abdallah
akisaini fomu za malipo kabla ya kukabidhiwa kizimbuzi chake pamoja na
Dish. Kulia ni Ofisa Idara ya Mauzo wa StarTimes, Joanna Nuhu.
Wananchi wakisubiri kulipia vizambuzi kabla ya kwenda kufungiwa.
Walimu wa Shule ya Msingi ya Yombo wakiwa na madishi yao wakienda kufungiwa baada ya kulipia.
…………………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Vizimbuzi ya StarTimes Tanzania imetoa vizimbuzi 50 kwa bei ya
sh.50,000 kwa vijiji vitatu vya Matimbwa, Chasimba na Yombo vilivyopo
Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vizimbuzi hivyo kwa wananchi wa
vijiji hivyo, Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Tang Jing Yu alisema lengo
lao kubwa ni kusogeza huduma ya kidigitali kwa wananchi.
“Kampuni
yetu imejipanga kuhakikisha inasaidia watu wa vijijini kupata huduma
nzuri na kuwanufaisha katika mfumo wa kidigitali” alisema Jing Yu.
Jing
Yu alisema kwa awamu ya kwanza wameanza kwa kusambaza vizimbuzi 50
chini ya mradi huo katika vijiji hivyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za
Rais wao wa China za kusaidia nchi za Afrika kidigitali hasa katika
maeneo ya vijijini.
Alisema
China inajisikia fahari kubwa kuona wananchi wa Afrika wananufaika na
mradi huo na kwa hapa Tanzania wameanza katika eneo hilo la Bagamoyo
lakini lengo likiwa ni kuvifikia vijiji vingi zaidi.
Ofisa
Idara ya Masoko wa StarTimes, Furaha Mayala alisema kabla ya kuanza
mradi huo waliwatembea wananchi na kuzungumza nao na kujionea changamoto
kubwa ya kukosa mawasiliano hayo ya kidigitali.
Alisema
kampuni hiyo imetoa vizimbuzi hivyo kwa watu 50 wa vijiji hivyo ambapo
watatumia kwa kipindi cha mwezi mmoja bila ya kulipia na amewataka
wananchi wengine kuchangamkia fursa hiyo.
Mgeni
rasmi katika hafla hiyo Ofisa Tarafa ya Yombo Rashid Kiwamba alisema
kupelekewa vizimbuzi hivyo kwa bei nafuu ni fursa kwao hasa katika
kipindi hiki cha sayansi na teknolojia ambapo dunia imekuwa ni kijiji
kimoja.
Kiwamba
alisema kwamba mradi huo uliopelekwa na StarTimes ni utekelezaji wa
ahadi ya Rais Dk.John Magufuli aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi
mkuu za kuhahikisha huduma mbalimbali zinawafikia wananchi ikiwa ni
pamoja na mawasiliano.
“Mradi
huu tulioletewa na hawa ndugu zetu wa StarTimes ni mzuri na ni mwanzo
mzuri na mambo mengi mazuri yanakuja hapa kwetu Yombo ni muhimu wananchi
kuuchangamkia” alisema Kawamba.
Mkazi
wa Kijiji cha Chasimba Miraj Mukadase aliishukuru kampuni hiyo kwa
kuwapelekea mradi huo ambao utawasaidia kupata taarifa mbalimbali kwa
wakati.
“Tulikuwa
tukikosa taarifa mbalimbali kwa kuwa tulishindwa kupata vizimbuzi vya
bei nafuu na vilivyobora ambapo vilikuwa vikuzwa hadi sh.120, 000 lakini
leo hii StarTimes wametukomboa tunawapongeza sana” alisema Mukadase.






0 maoni:
Chapisha Maoni