Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai
akizungumza kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango hajawasilisha
Mapendekezo ya kiwango na ukomo wa Bajeti ya serikali kwa mwaka
2016/2017 wakati wa mkutano wa Wabunge wote uliofanyika ukumbi wa
Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mpiango Dkt
Philip Mipango akiwasilisha Mapendekezo ya kiwango na ukomo wa bajeti
kwa mwaka 2016/17 wakati wa mkutano wa Wabunge wote uliofanyika ukumbi
wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim
akiongoza kikao cha Wabunge wote wakati Serikali ilipowasilisha
mapendekezo ya kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/17.
Kulia kwake ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai na kushoto ni Naibu Spika
Dkt Tulia Ackson.
(Picha na Ofisi ya Bunge)






0 maoni:
Chapisha Maoni