Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiana Lubuva akisalimiana na Catographia Bwana
Brian Mhonda toka Tume ya Uchaguzi Zimbabwe walipofika ofisi kwake
kusalimiana naye. Katikati toka kushoto ni Kaimu Mkuu wa sehemu ya
Catographia toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Adolph Kinyero na Afisa
Uchaguzi wa Wilaya Toka Tume ya Uchaguzi Zimbabwe Collins Chamunorwa
Muchenjekwa
………………………………………………………………………………………………………………………..
Na Christina Njovu-NEC
Ujumbe kutoka Tume ya Uchaguzi ya
Zimbabwe (ZEC) umekuja kujifunza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
jinsi ilivyoendesha zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura kwa kutumia Mfumo
wa Biometrick Voter Registration (BVR) kwa kuwa Tanzania ilifanikiwa
kwa kiasi kikubwa kuandikisha wapiga Kura wengi kwa kutumia technologia
hiyo mpya.
Wakizungumza na Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji Mstaafu Damian Lubuva ujumbe huo wa
watu wawili Brian Mhonda na Collins C. Muchenjekwa toka Tume ya Uchaguzi
ya Zimbabwe wameeleza kuwa; Zimbabwe ipo katika maandalizi ya
kuandikisha Wapiga Kura.
Ujumbe huo umeeleza kuwa;
Zimbabwe imeichagua Tanzania nchi ambayo imefanya uandikishaji wa Wapiga
Kura hivi karibuni na kufanikiwa kuandikisha watu wengi kwa muda mfupi
kwa kutumia mfumo wa BVR.
“Tupo katika maandalizi ya
kuandikisha Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voters
Registration (BVR) mfumo ambao Tume yetu imeuchagua kutokana na kukua
kwa Technolojia duniani” Mfumo huu kwa Zimbabwe utatumika kwa mara ya
kwanza” alisema bwana Muchenjekwa.
Wakiwa katika Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) ujumbe huo ulijifunza namna Elimu ya Mpiga Kura
ilivyotolewa kiasi cha kuwafikia watu wengi ambao walijitokeza
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Katika Ziara hiyo ya
mafunzo,wajumbe hao walihitaji kujifunza zaidi njia na mbinu mbalimbali
za kutoa Elimu ya Mpiga Kura ili iweze kuwafikia wananchi wengi ili
wajitokeze kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Sambamba na hilo walijifunza
namna ya kusoma ramani ya Majimbo ya Uchaguzi na Jinsi gani Tume
ilifanya manunuzi ya vifaa vya Uandikishaji wa Wapiga Kura.
Ujumbe huo ulijikita zaidi katika
kujifunza jinsi Biometrick Voter Registration (BVR) namna inavyofanya
kazi pamoja na changamoto zake.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewapongeza kwa kuchagua kuja
kujifunza nchini Tanzania kwani kitendo hicho kinaipa heshima NEC na
Tanzania kwa ujumla.






0 maoni:
Chapisha Maoni