Msemaji
wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa
huo leo.
Msemaji
wa CCM, Mjune wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Katibu wa
CCM mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndakubali baada ya kuwasili Ofisi ya CCM
mkoa wa Manyara kuanza ziara ya kikazi mkoani huo leo
Katibu
wa CCM mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndakubali akimkaribisha Mjumbe wa NEC,
Kilumbe Ng’enda alipowasili Ofisi ya CCm mkoa huo leo akifuatana na
Msemaji Mkuu wa CCM Christopher ole Sendeka katika ziara ya kikazi leo
Msemaji
wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na baadhi
ya viongozi alipowasili ofisi ya CCM mkoa wa Manyara leo kuanza ziara ya
kikazi
Msemaji
wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akifuatana na Katibu
wa CCM mkoa wa Manyara Ndakubali, wakati akitoka katika Ofisi ya CCM
mkoa huo, tayari kwenda Wilaya ya Babati kuhutubia mkutano wa habadhara
leo
Msafara wa Msemaji wa CCM na Mjumbe wa NEC, Ole Sendeka ukienda Babati
Msemaji
wa CCM na Mjumbe wa NEC, Ole Sendea (kushoto), akilakiwa na kinamama wa
Kata ya Bashneti alipowasili kuhutubia mkutano wa habadhara katika kata
hiyo wilayani Babati leo.
Shamrashamra za kumsindikiza Ole Sendeka kwenda meza kuu
Msemaji
Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimia baadhi
ya wananchi na viongozi wa CCM wilaya ya Babati baada ya kuwasili
katika Kata ya Bashneti, kuhutubia mkutano wa hadhara leo.
Msemaji
Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akiwasailimia
waasisi wa Chama katika wilaya ya Babati alipowasili Kata ya Bashneti
wilayani humo mkoani Manyara leo
Msemaji
Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akiwasailimia
wananchi kwa kuwapungia mkono alipowasili Kata ya Bashneti wilayani humo
mkoani Manyara leo
Katibu
wa CCM wilaya ya Babati Vijijini, KhabasMwijuki akitoa maneno ya
utanguliza baada ya Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher
Ole Sendeka lipowasili Kata ya Bashneti wilayani humo mkoani Manyara
leo
Baadhi
ya waasisi wa TANU na baadaye CCM wakiwa kwenye mkutano wa Msemaji Mkuu
wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka uliofanyika Kata ya
Bashneti wilayani humo mkoani Manyara
Msemaji
Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akivishwa vazi la
wazee wa Kabila la wairaq, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika
kata ya Bashneti wilayani Babati mkoani Manyara leo
Kina
mkereketwa akiwa na picha ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere
kwenye mkutano hu wa Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher
Ole Sendeka katika Kata ya Bashneti wilayani Babati nmkoani Manyara leo
Msemaji
Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akiwa na wazee wa
kimila ya kabila la Iraq, kabla ya kuhutibia mkutano wa hadhara katika
kata ya Bashneti wilayani Babati mkoani Manyara leo
Kina mama wakiwa katika shangwe wakati wa mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika kata ya Bashneti
Mzee wa kimila akiombea dua ya kimila mktano huo wa hadhara
Mwenyekiti
wa CCM Kata ya Bashneti Beda Lukoa akimkaribisha Msemaji Mkuu wa CCM na
Mjumbe wa NEC Christopher Ole Sendeka kwenye mkutano huo
Diwani wa Kata ya Bashneti Jovita Mandoo akieleza mikakati ya Kata hiyo iliyopangwa kuleta maendeleo
Msemaji
Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC< Christopher Ole Sendeka akiperuzi
ilani ya CCM, kabla ya kupanda jukwaani kuhutubia mkutano wa hadhara.
Msemaji
Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na
Karoli Oli, aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa TANU kata ya Bashnet tangu
mwaka 1962, baada ya kutambukishwa kwake katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kata hiyo leo
Katibu
wa CCM mkoa wa Manyara akiendelea na utaratibu jukwaani kabla ya Ole
Sendeka kuhutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Bashneti
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wialaya ya Mbulu mkoani Manyara, akimsalimia Msemaji
Mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka wakati wa mkutano huo wa hadhara
uliofanyika Kata ya Bashneti. Kulia ni Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng’enda
aliyeko katika ziara hiyo ya Msemaji Mkuu wa CCM.
Mjumbe
wa NEC, Kilumbe Ng’enda akifungua pazia kwa kutoa hotuba fupi, kabla ya
Msemaji Mkuu wa CCM, Chrstopher Ole Sendeka kuhutubia mkutano huo wa
hadhara uliofanyika kata ya Bashneti, Babati mkoani Manyara leo
Msemaji
Mkuu wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akihutubia mkutano
wa hadhara uliofanyika leo katika Kata ya Bashneti, wilayani Babati
mkoani Manyara.
amesema, Chama Cha Mapinduzi kinamuunga mkono na kumtetea kwa nguvu zake zote Rais Dk. John Magufuli katika jitihada zake za kuliinua taifa la Tanzania.
Amesema, CCM itafanya hivyo kwa sababu kazi anayofanya ya kupambana na wazembe na wezi wa mapato kwenye vyanzo vya uchumi wa taifa inatokana na maelekezo ya ilani ya CCM.
Sendeka amesema, CCM inawataka wale wote wanaojaribu kupotosha jitihada zinazofanywa na Rais za ‘kupasua majipu’, kuwa ni kuwaonea wanaochukuliwa hatia, kuacha mara moja, kwa sababu kinachofanyika ni sahihi na kwa mujibu wa sheria.
Amesema, upasuaji majipu huo unaofanaywa na Rais Magufuli hauchagui bali yeyote anayebainika kuwa ni jipu hata akiwa mwana CCM haachwi.
Kwa upande wake, Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng’enda, amewataka Watazania kutambua kuwa Uchaguzi umeshamalizika kwa hivyo asitokee yeyote kuanza kuweweseka, kwa kutoa maneno ya kejeli kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli kwa sababu baada ya uchaguzi kumalizika sasa kiichobaki ni kuchapa kazi.
Amsema, hakuna sababu za mwanasiasa yeyote kuanza mambo ya fitina za kisiasa wakati huu kwa kuwa kufanya hivyo anajisumbua.

0 maoni:
Chapisha Maoni