Wachezaji wawili wenye miili
midogo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Farid Mussa wamekuwa waokozi wa
Azam FC baada ya kila mmoja kufunga bao moja na kutoa pasi ya moja.
Singano na Farid,
kila mmoja alifunga baada ya kupewa pasi na mwenzake wakati Azam FC
ilipoichapa Esperance ya Tunisia kwa mabao 2-1 katika mechi ya Kombe la
Shirikisho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Tayari wakongwe John
Bocco ambaye ni nahodha na mkongwe mwingine, Kipre Tchetche walishindwa
kabisa kuonyesha cheche baada ya kupoteza zaidi ya nafasi nne za
kufunga.SOURCE http://salehjembe.blogspot.com/2016/04/taswira-tano-azam-ikiitoa-shoo.html






0 maoni:
Chapisha Maoni