Ijumaa, 8 Aprili 2016

NAIBU WAZIRI WA UJENZI AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO KWA SEKTA YA UCHUKUZI.


1Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (kulia), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leornard  Chamuriho, kabla ya ufunguzi wa mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi, linalofanyika Katika Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
2Baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, wakitambulishwa katika mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa sekta hiyo.
3Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, akitoa hotuba yake katika mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi, linalofanyika Katika Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
4  Wajumbe wa Mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi, wakimsikiliza, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi.6Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Sekta ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi.
7Meneja wa Kituo cha TCAA, Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Bw. John Chambo akimwonyesha Naibu Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani( kushoto), ramani inayoonyesha njia za ndege, wakati alipotembelea ofisni hapo.
5Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (wa tatu kutoka kulia mstari wa kwanza), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Uchukuzi, linalofanyika Katika Ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

0 maoni:

Chapisha Maoni