Mshukiwa
muhimu wa shambulio la kigaidi la mwezi Novemba mjini Paris ,Mohamed
Abrini amekamatwa,vyombo vya habari vya Ubelgiji vimesema.
Duru za
vyombo hivyo vya habari zinasema kuwa Abrini ni mtu anayeshukiwa kuvaa
kofia aliyeonekana katika kanda ya CCTV kabla ya mlipuko katika uwanja
wa ndege wa Brussels mnamo tarehe 22 mwezi Machi.
Waendesha mashtaka wamethibitsha kwamba watu kadhaa walikamatwa kuhusiana na shambulio hilo la Brussels.
Image copyrightEPAImage captionPicha ya Mohamed Abrini
Shambulio hilo la Paris mnamo mwezi Novemba liliwaua watu 130.
Vyombo
vya habari vinasema kuwa Abrini ambaye amekuwa mafichoni kwa takriban
miezi mitano alikamatwa wilayani Anderlecht huko Brussels.
0 maoni:
Chapisha Maoni