Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani Dau.
NA MWANDISHI WETU Risasi Jumamosi
“Hili
jambo halikubaliki na kama tuhuma hizi ni za kweli, basi tunamuomba Rais
John Magufuli amchukulie hatua za kisheria kama wanavyofanyiwa wakubwa
wengine waliolitia taifa letu hasara. Hiki ni kiasi kikubwa cha fedha
ambacho kingeweza kutumiwa kutatua kero mbalimbali zinazotukabili
Watanzania,” alisema msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Seve Nyari
kutoka Singida.
Joji
Salum, aliyepiga simu kutoka Kigamboni, Dar alisema ni kweli mradi wa
ujenzi wa Jiji Jipya la Kigamboni umesimama na hawajui ni kwa sababu
gani, lakini kwa ufisadi wa fedha zinazotajwa, hakuna jinsi zaidi ya
kumsulubu Dau ambaye aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa balozi lakini bado
hajapangiwa kituo cha kazi kwa sababu alishiriki kwa asilimia mia moja
si kwa kuzichukua bali kama mtendaji mkuu.
Kutoka Arusha, ambako NSSF inaendelea na mradi mwingine wa ujenzi wa nyumba wilayani Arumeru, Maige Joseph alisema:
Kutoka Arusha, ambako NSSF inaendelea na mradi mwingine wa ujenzi wa nyumba wilayani Arumeru, Maige Joseph alisema:
“Wakati
umefika kwa mifuko ya jamii kama huu, kudhibitiwa katika uanzishaji wa
miradi yake, kwani mingi ni ya kifisadi yenye kuwanufaisha wakubwa.
“Sasa mtu
una ardhi yako, lakini unanunua tena ya mtu mwingine, tena kwa bei
ghali zaidi. Yaani unatoka kilometa 30 kutoka Arusha mjini, unakwenda
kununua heka moja kwa shilingi bilioni moja!? Hii haijapata kutokea,
labda Tanzania tu. Wasulubiwe walioshiriki,” alisema Maige.
Akaongeza:
“Nasema Dau anahusika kwa sababu si ndiyo alikuwa bosi mkuu? Maana yake
ni kwamba hakuna kilichokuwa kikifanyika bila ya yeye kujua. Ni lazima
anajua mwanzo mwisho. Mimi naona hata huo ubalozi ungetenguliwa tu kwani
ameacha doa NSSF.”
Kauli ya kutaka watu wote waliohusika kufisadi fedha hizo wasubulubiwe, pia ilitoka kwa wananchi waliopiga simu kutoka Mwanjelwa Mbeya, Tukuyu (pia Mbeya), Iringa mjini, Mtwara, Simiyu, Kondoa (Dodoma), Tanga na Mwanza.
Kauli ya kutaka watu wote waliohusika kufisadi fedha hizo wasubulubiwe, pia ilitoka kwa wananchi waliopiga simu kutoka Mwanjelwa Mbeya, Tukuyu (pia Mbeya), Iringa mjini, Mtwara, Simiyu, Kondoa (Dodoma), Tanga na Mwanza.
Ufisadi
ulioibuliwa hivi karibuni ni kiasi cha shilingi trilioni 1.3 kinadaiwa
kutumiwa na NSSF katika mazingira yanayotia shaka katika ununuzi wa
ardhi ili kutekeleza miradi miwili ya ujenzi wa nyumba huko Kigamboni na
Arumeru mkoani Arusha. Jijini Dar es Salaam, mfuko huo ulianzisha mradi
uitwao Dege Eco Village ambao Bodi ya NSSF iliunda Kampuni ya Hifadhi
Builders inayosimamia ujenzi huo ikishirikiana na Kampuni ya Azimio
Housing Estate Limited.
Inadaiwa
Azimio Housing Estate inayomiliki ekari 20,000 huko Kigamboni, iliiuzia
NSSF eneo la ekari 300 kwa shilingi milioni 800 kwa ekari moja, badala
ya bei halali ya shilingi milioni 39 kwa ekari tofauti na bei
iliyotangazwa na Manispaa ya Temeke mwaka 2012 wakati ikiuza eneo lake
kwa shilingi elfu nane kwa mita ya mraba.
Katika
ujenzi wa Arumeru, inadaiwa kampuni hiyo ya Azimio, iliiuzia NSSF ekari
moja kwa shilingi bilioni 1.8, wakati bei halisi ya ukubwa huo kwa
mujibu wa wakazi wa eneo hilo lililo umbali wa zaidi ya kilometa 30
kutoka jijini Arusha, ni kati ya shilingi laki tano hadi milioni moja.
Uchunguzi
unaonesha Azimio iliuza eka 300 za Kigamboni kwa dola 108, 906,113
(sawa na madafu bilioni 217.8), wakati huko Arumeru mfuko huo uliuziwa
ekari 655 kwa dola 556, 764, 924 (trilioni 1.13) na hivyo kuifanya jumla
ya fedha ambazo ‘zimeliwa’ katika miradi hiyo miwili katika ardhi peke
yake kufikia trilioni 1.3.






0 maoni:
Chapisha Maoni