| Mkazi wa Kidamali Iringa Bw Joseph Balami akiwa ametiwa hatiami kwa kuhukumiwa kunyogwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauwaji |
.................................................................................................................................................................................
MKAZI
wa Kidamali wilaya ya Iringa mkoani Iringa Bw Joseph Balami
amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya
kumua Stani Singaile (42) kwa kumchoma kisu kusudi wakati wa ugomvi
uliotokea kwenye klabu cha pombe za kienyeji .
Hukumu hiyo imetolewa leo na mahakama kuu
kanda ya Iringa imetoa baada ya kuridhishwa na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo na upande wa jamhuri ambao ulidai kuwa
mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Oktoba 15 mwaka
2011 katika kijijhi cha Kidamali kwa kumuua
Stani Singaile (42) .
Stani Singaile (42) .
Akisoma hukumu hiyo,Jaji Mfadhi
wa mahakama Kuu kanda ya Iringa Bi Mary Shangali alisema katika shauri kesi hiyo
amekubaliana na upande wa mashitaka ulidai ushhidi uliotolewa mahakamani udhihirisha
pasipo shaka kuwa mtuhumuwa alitenda kosa hilo.
“Katika kesi hii
upande wa mashitaka ulileta mashidi watano na upande wa utetezi ulileta
mashahidi wawili ambao ni mtuhumiwa mwenywe na mke wake waliotoa ,ushahidi mahakamani,mahakama
imekubaliana na upande wa mashitaka kuwa mtuhumuwa ametenda kosa na imemtia
hatiani kwa kosa la kuua kwa makusudi”alisema Shangali na kuongeza:
"Kwa kuwa adhabu
inayotolewa kwa kosahilo ni moja kwa mjibu wa sheria...,ninakuhukumu
kunyongwa hadi kufa”alisema Shangali.
Awali kabla ya
Hakimu kusoma hukumu hiyo mawakili Felix
Chakela upnde wa serikali na Lwezaula Kaijage upande wa utetezi walipewa nafasi
ya kutoa hoja zao ambapo Chakela aliitaka mahakama kumpa adhabu kali mtuhumiwa
ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo
wakati Lwezaula alisema anasubiri hukumu ya mahakama.
Awali Jaji huyo
aliyekuwa akinukuu maelezoya awali ya kesi hiyo iliyofunguliwa mahgakamani hapo
na wawili wa serikali …alidai mtuhumiwa
alitendokosa hilo Oktoba 15 mwaka 2011 katikakilab cha pombe za kienyeji.
Alisemakulingana na
mashuhuda waliotoaushahidi mahakamani pa wamethibitsiha bilakuacha shakakuwa
siku hiyo mtuhumiwa alikwenda kwenye kilabu kile na kumfuatamarehemu kisha
kumchoma na kisu kifuani.
Alisema kitendo cha
mtu kumfuata mtu na kumchoma kisu kifuani hususani upande wa kushoto
kinaonyesha alidhamilia kua na kwamba kwatendohilomahakamainamtia hatini
kwakosala mauaji ya kukusudia.
Pia aliongeza kuwa
ushahidi uliotolewa mahakamani hapo
pamoja na maoni yaliyotolewa na waungwana wa mahakama yanakubaliana kuwa
ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukuacha shaka kwa mtuhumiw
akuhusika na tukio hilo.
Katika kesi
hiyo mtuhumuwaBw Balami anadaiwa kuwa Oktoba 15 mwaka 2011katika kijiji cha
Kidamali Wilaya ya Iringa majira ya saa moja usiku alimua Singaile kwakumchoma
na kisu ,tukio alilotenda kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.
Alidawa
mahakamani
hapa na uapnde wa jamuhuri kuwa baada ya tukiomtuhumiwa alikimbia lakini
alikamtwa majiraya saa mbili usiku na kufikishwa kwenye ofisi ya
serikali ya
kijiji na baadae katika kituocha polisi kwa hatua zaidi hata hivyo
mahakama hiyo imesema kuwa rufaa kwa ipo wazi kwa mshitakiwa
huyo.







0 maoni:
Chapisha Maoni