Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa
Taifa wa mwezi Machi 2016 na kusema kuwa umepungua kidogo hadi kufikia asilimia
5.4 kutoka asilimia 5.6.iliyokuwepo mwezi Februari, 2016.
Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi Machi 2016 imepungua
kidogo ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma iliyokuwepo mwezi Februari mwaka huu.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akitoa taarifa ya Mfumuko wa
Bei wa Mwezi Machi, 2016 leo jijini Dar
es salaam amesema kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa
bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali
nchini.
Amesema Takwimu zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania
Bara Machi 2016 kwa mujibu wa bei za bidhaa zilizoainishwa kupima mfumuko wa
bei zinaonyesha kuwa bidhaa zisizo za vyakula katika soko zikiwemo Gesi, dizeli
na mafuta ya taa zimechangia kupungua kwa mfumuko huo.
Amesema kuwa pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei
ya bidhaa hizo mwezi Machi mwaka huu baadhi ya bidhaa za vyakula zikiwemo za mchele,
Mahindi, vyakula kwenye Migahawa na mkaa zimeonesha kuongezeka katika soko.
Kuhusu Fahirisi za
Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na
huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania kwa mwezi Machi, Kwesigabo amesema
kuwa zimeongezeka hadi kufikia 101.93 kutoka 101:44 za mwezi Februari.
Amesema baadhi ya bidhaa za vyakula za vyakula zikiwemo unga
wa muhogo, matunda, maharagwe na samaki zimechangia kuongezeka kwa Fahirisi
hizo na kuongeza kuwa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia ongezeko hilo ni Mavazi
ya wanawake, mkaa na kuni.
Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika
kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Machi , 2016 umefikia shilingi 98 na senti 11 ikilinganishwa na uwezo wa shilingi 98 na senti 58 wa mwezi Februari
2016.
“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania
katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Machi 2016
umepungua, hii ina maana kuwa sasa mtu kuongeza ziada ili aweze kununua bidhaa
na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Februari"
Kwa upande wa
mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki mwezi
Machi, 2016, Kwesigabo amesema una mwelekeo unaofanana; Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 6.45 kutoka 6.84 huku
Uganda ukifikia asilimia 6.2 kutoka asilimia 7.0 za mwezi Februari.






0 maoni:
Chapisha Maoni