Ijumaa, 8 Aprili 2016

IRUWASA YAKABIDHI MNRADI WA MAJI ILULA KILOLO , MBUNGE MWAMOTO ACHUKIZWA NA WANASIASA KUINGILIA UTENDAJI

............


Mwenyekiti  ya  bodi ya maji ya  mamlaka ya maji  safi na maji taka  mjini Iringa (IRUWASA) Paschal Mhongole (kulia) akimkabidhi mwenyekiti wa maji mji  wa Ilula Bi Anna kabuje nyaraka  za mradi wa maji wa Idemule kwa ajili ya wananchi wa kata  tatu  za mji  wa Ilula mradi  uliojengwa kwa nguvu ya wizara ya maji na umwagiliaji kwa zaidi ya Tsh milioni 860 anayepiga makofi  katikati ni  mbunge wa jimbo la Kilolo Bw  Venance Mwamoto
Viongozi na wananchi wa kata  tatu za Ilula  wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa maji wa Idemule
Mwenyejkiti wa bodi ya IRUWASA Bw Mhongole kushoto akiwa na mbunge wa  jimbo la Kilolo Bw Venanve  Mwamoto
MkurugenzI wa IRUWASA Bw Gilbert Kayange  akikabidhi  taarifa  ya mradi huo wa maji Ilula
Mkurungezi wa IRUWASA Bw Gilbert Kayange akitoa  taarifa ya mradi huo 
kaimu meneja  wa mradi wa maji Ilula Bi Mvungi kushoto  akiwa katika  hafla  hiyo
Zoezi la  kusaini hati ya makabidhiano  likiendelea
Baadhi ya maeneo ambayo mradi huo umekuwa  ukihujumiwa  
MAMLAKA  ya  maji  safi na maji taka  mjini Iringa (IRUWASA )  imekabidhi maradi  wa maji wa maji   uliogharimu kiasi cha  Tsh milioni 903kwa mamalaka  ya maji ya  mji  mdogo  wa Ilula  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa baada ya mradi  huo ujenzi  wake  kukamilika   huku mbunge  wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto akitaka  wanasiasa kuacha  kushikilia andiko la mradi mkubwa wa maji katika mji  wa  Ilula

 Akizungumza katika  hafla ya makabidhiano ya mradi   huo wa maji jana mbunge  wa  jimbo la  Kilolo Bw Mwamoto pamoja na  kupongeza wizara ya  maji na  umwagiliaji kwa  kusaidia  kutoa  pesa  kwa  ajili  ya mradi  huo bado alieleza kusikitishwa  kwa na hatua ya wanasiasa  katika wilaya ya Kilolo kushikilia andiko la mradi mkubwa wa maji katika  mji  huo na  kutaka nyaraka zote  za miradi kuhifadhiwa na wataalam  na sio  wanasiasa .
Kwani alisema  kuwa moja kati ya mambo ambayo  yanachelewesha ufumbuzi  wa  kudumu  wa kero ya maji katika mji  wa Ilula  ni pamoja na baadhi ya wanasiasa kuingiza siasa katika shughuli za  kimaendeleo na kutaka maandiko yote ya  miradi ya maji katika  wilaya ya Kilolo ambayo yaliandikwa kabla ya yeye  kuwa  mbunge  wa  jimbo  hilo kukabidhiwa na kuhifadhiwa na watendaji  wa mamlaka ya maji na  si vinginevyo.
Mbunge  huyo  alisema  kuwa haungi mkono wazo  la andiko  la  kutoa  maji kwa  ajili ya mradi mkubwa kutoka  chanzo cha maji  cha  Idemule kwani mradi  huo ni vigumu kutekelezeka na  kuwa ni  vema mradi mkubwa wa maji kwa  ajili ya  wananchi wa mji wa Ilula ukatekelezwa  kutoka mto Ruaha mjini Iringa  kuliko kutegemea chanzo  hicho cha Idemule  .
Alisema  kuwa tayari  Rais Dr  John Magufuli aliahidi kusaidia kutatua  kero ya maji katika  mji  wa Ilula wakati  wa kampeni  zake ila iwapo viongozi  wa maji na  wale  wa wilaya hiyo hawatakuwa wabunifu kwa kuangalia uwezekano wa  kutoa maji mto  Ruaha mjini Iringa na kubaki na mawazo ya  wanasiasa ya  kutaka maji hayo  kutoka mto Idemule  upo  uwezekano  wa Rais kumaliza muda  wake Ikulu  pasipo mradi  huo kutekelezeka .
"Naomba  kuwa wazi katika  hili   wapo baadhi ya  wanasiasa wanataka  kukwamisha  mradi huo mkubwa wa maji katika mji wa Ilula haiwezekani  kwa  mamlaka ya maji Ilula kumwachia mwanasiasa  kutunza andiko la maji wakati  si jukumu lake ...siasa inayoendelea Ilula na wilaya ya kilolo haina faida yeyote kwa  wananchi ......hivyo  ili mradi huu mkubwa uweze  kutekelezeka  kwa  wakati ni vema wataalam kuachwa kufanya kazi  za kitaalam na  wanasiasa  kufanya  siasa "
Alisema  kuwa sida kubwa hata ya miuondombinu ya maji katika mradi huo  kuendelea  kuhujumiwa ni siasa  chafu  zinazofanywa na baadhi ya  wanasiasa kwa ajili ya kinyongo cha  kukosa nafasi walizotegemea katika siasa .
Akitoa  taarifa ya  mradi huo mkurugenzi  wa IRUWASA Bw Gilbert Kayange  alisema  kuwa mradi   huo  utahudumia kata  tatu za mji  wa Ilula ambazo ni Nyalumbu , Ilula na Lugalo ambapo  wakazi 38,265 ambao  alikuwa wakikabiliwa na kero  ya maji kabla ya wizara ya maji na umwagiliaji  kutoa  kiasi cha Tsh milioni 860   kwa ajili ya kutatua kero  hiyo na  kuwa hadi sasa mradi huo unadaiwa kiasi  cha tsh milioni 43ambazo ni pesa kwa ajili ya kumlipa  mkandarasi wa  ujenzi wa mradi  kutokana na kazi alizofanya .

0 maoni:

Chapisha Maoni