Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la
Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), inatarajiwa kufanyika kesho
Jumanne saa 3 usiku moja kwa moja (live) kupitia kituo cha luninga cha
AzamTwo.
Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la
Shirikisho (ASFC) itafanyika live katika kituo cha AzamTwo, ambao
kupitia Azamtv ndio wadhamini wa wakuu wa michuano hiyo iliyoibua
msisimiko wa mpira wa miguu na kushirikisha timu nyingi zaidi nchini.
Baada ya timu za Azam FC, Mwadui
FC, na Yanga SC kukata tiketi ya kucheza Nusu Fainali, mshindi wa mchezo
kati ya Simba SC dhidi ya Coastal Union utakaochezwa leo katika uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam atungana na timu hizo tatu kwenye droo ya
kesho.
Michuano ya Kombe la Shirikisho
iliyoanza kwa kushirikisha timu 64 mwishoni mwa mwaka jana, imefikia
hatua hatua ya nusu fainali, baada ya Azam FC kuindoa Prisons (3-1),
Mwadui FC kuiondosha Geita Gold (3-0) na Yanga SC kuwaondoa Ndanda FC
kwa mabao (2-1).
Mshindi wa Kombe la Shirikisho
(ASFC) msimu huu, ataiwakilisha Tanzania mwaka 2017 katika michuano ya
Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC).






0 maoni:
Chapisha Maoni