Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na
waandishi wa habari ambao hawapo pichani kuhusu ugonjwa wa kipindupindu
kwa mujibu wa takwimu za wiki iliyopita kuanzia Aprili 4 hadi 10 mwaka
huu, ambapo wagonjwa walioripotiwa ni 368 ikilinganishwa na za wiki ya
Machi 28 hadi Aprili 3, mwaka huu idadi ya wagonjwa walioripotiwa
ilikuwa 531.Hivyo jumla watu wagonjwa walioripotiwa tangu ugonjwa huo
uanze ni 20,655 na waliopoteza maisha ni watu 326.
Picha kwa hisani ya Wizara ya Afya.






0 maoni:
Chapisha Maoni