Na Mwandishi wetu , Zanzibar.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
kimesema kitaendelea kuimarisha miundombinu na mazingira rafiki ya
kiutendaji kwa kuwapatia vifaa vya kisasa jumuiya mbali mbali za taasisi
hiyo ili zifanye kazi kwa ufanisi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar, Najma Murtaza Giga wakati
akikabidhi Vifaa mbali mbali kwa Uongozi wa Wazazi Mkoa wa Mjini, huko
Afisi ya CCM Amani.
Amesema taasisi hiyo inatakiwa kwenda sambamba na mabadilio ya sayansi na teknolojia kwa kutumia nyenzo za
kisasa zitakazowasaidia watendaji wa taasisi hizo kufanya kazi nzuri na kwa haraka.
kisasa zitakazowasaidia watendaji wa taasisi hizo kufanya kazi nzuri na kwa haraka.
Aidha amesema chama hicho
kitafanya kila kinachowezekana kuhakikisha kinawapatia Vitendea Kazi
Watendaji wa CCM kadri ya uwezo wa kifedha unaporuhusu.
Giga amewasihi viongozi mbali
mbali wa chama na jumuiya zingine kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
jumuiya ya wazazi katika kutoa malezi bora ya kitaaluma na kisaikolojia
kwa watoto kwa lengo la kutengeneza viongozi makini na weledi wa baadae.
Nae Katibu wa CCM mkoa wa mjini,
Mohamed Omar Nyawenga amewataka watendaji wa chama hicho kuwa wabunifu
na kutumia weledi kwa kufanya kazi kwa bidi ili kusaiudia chama
kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2015/2020 kwa ufanisi ili wananchi
waendelee kuiunga mkono CCM katika chaguzi zote zijazo.
Vifaa vilivyotolewa ni Komputa 2, mashine za Printer 2 na mashine za photocopy 4 kwa jumuiya ya wazazi mkoa wa mjini kichama.






0 maoni:
Chapisha Maoni