Jumamosi, 10 Septemba 2016

WANAFUNZI ST. JOSEPH WACHANGIA DAMU MUHIMBILI LEO, WENGI WATAKIWA KUJITOKEZA

Posted  by Esta Malibiche on Sept10.2016 in News
1
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Joseph Cathedral School High School jijini Dar es Salaam wakichangia damu LEO katika shule hiyo.
2
Wanafunzi wa shule hiyo wakijiandikisha kabla ya kuchangia damu leo.
3
Renatha Temu akichukua damu kutoka kwa  Imelda Daniel Mtuka ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo.
4
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakisubiri kuchangia damu leo asubuhi.
5
Damu ikiwa imetunzwa kwenye chupa maalumu baada ya baadhi ya wanafunzi kuchangia leo.
6
Ofisa Mhamasishaji wa Damu Salama katika hospitali hiyo, Hamisi Omari akimpima wingi wa damu Collin Mneney wa kidato cha tano katika shule hiyo.
7
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakichangia damu leo.
Na John Stephen
Dar es Salaam, Tanzania. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Joseph Cathedral School High School jijini Dar es Salaam leo wamechangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye mahitaji ya damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Shughuli ya utoaji damu imefanyika katika shule hiyo leo asubuhi na zaidi ya lita 77 zimepatika kutoka kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mmoja wa wanafunzi waliochangia damu leo, Imelda Daniel Mtuka anayesoma kidato sita amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa kwenye hospitali hiyo.
“Siku ya leo najisikia mwenye furaha sana kwa kuwa nimechangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa,” amesema Imelda.
Naye John Mselle ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo amewataka Watanzania hasa wanafunzi wa shule mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangia damu.
“Nawaomba wanafunzi shule za sekondari na vyuo vikuu kujitokeza kwa wingi kuchangia damu. Wanafunzi wenzangu wawe na moyo wa kusaidia maana hawajui leo au kesho, inawezekana kwamba ndugu yake anahitaji damu,” amesema Mselle.

0 maoni:

Chapisha Maoni