Jumamosi, 10 Septemba 2016

Tetemeko Ardhi lenye Nguvu ya 5.7 labomoa Nyumba Mkoani KAGERA

Posted by Esta Malibiche on Sept 10.2016 in NEWS

4

Nyumba kadhaa katika Mkoani Kagera zimebomoka baada ya tetemeko la Ardhi lenye nguvu ya 5.7 kipimo cha Ritcher kupita kwenye mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa.

Taarifa zinadai Mji wa Kamachumu Mkoani Kagera ndio umeathiriwa Vibaya na tetemeko hilo, ambapo nyumba nyingi zimebomolewa.

Hadi sasa hakuna idadi ya vifo au Majeruhi iliyotolewa na Mamlaka zinazohusika mkoani Kagera.

Mtandao wa www.habari360.com unaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa za tukio hilo.

Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini Bukoba likiwa katika harakati za Uokoaji.
Nyumba Moja wapo ambayo imeathirika na Tetemeko hilo lililotokea Muda mfupi uliopita Mjini Bukoba.
Nyumba ikionekana kupata nyufa baada ya tetemeko la Ardhi kuutikisa Mji wa Bukoba hivi Punde.
Milango ya Geti katika nyumba hiyo ikionekana kuanguka chini baada ya kukumbwa na dhoruba ya tetemeko la Ardhi, lililotikisa Mji wa Bukoba.
Baadhi ya Nyumba za Wananchi wa Mji wa Bukoba Zikiwa katika hali Mbaya baada ya Tetemeko la Ardhi Kupita.
Add caption








0 maoni:

Chapisha Maoni