…………………………………….
Hospitali zinazotumia mfumo.wa ukusanyaji mapato wa kielectronik wametakiwa wasibweteke na mapato wanayoyakusanya kila siku.
Hospitali zinazotumia mfumo.wa ukusanyaji mapato wa kielectronik wametakiwa wasibweteke na mapato wanayoyakusanya kila siku.
Rai
hiyo.imetolewa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na
watoto Mh.Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya kanda
ya mjini Mbeya
Ummy
alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa
katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ununuzi wa dawa,vifaa na
vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa watumishi
“Bado tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote,tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa”alisema
“Bado tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote,tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa”alisema
Aidha alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa
itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma,hivyo
wameishauri bohari kuu ya dawa wanunue dawa toka kwa wawekezaji wa hapa
nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji wa
dawa kwa haraka
waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia,kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa
“Tunao watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa na
kuzipeleka kwenye maduka ya.dawa binafsi,hao hatutowafumbia macho na
kuwapeleka mahakamani”
Kuhusu upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini ,Wazirini wa afya
alisema,nchi ina upungufu wa asilimia 52,hivyo.serikali inatarajia
kuajiri watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa
nchi nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni
Katika hospitali ya uzazi ya Meta,waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi
za wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na
wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka
ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na
watoto njiti
Hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha
shilingi mia tano,inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya
watu milioni mbili.






0 maoni:
Chapisha Maoni