WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa
Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa dawa za kulevya
atakayetoweka katika gereza la
mkoa huo.
mkoa huo.
Amesema kuna watuhumiwa wa dawa
za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la mkoa wa Lindi hivyo ni
vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao
umeimarishwa.
Hata hivyo, Waziri Mkuu, Majaliwa
amemtaka mkuu wa gereza hilo kuwa makini na baadhi ya zabuni
wanazozitoa kutoka nje na kuhakikisha ulinzi unaimarisha wakati wote
gerezani hapo.
Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema
hayo jana (10 Aprili, 2016) wilayani Ruangwa wakati akipokea taarifa ya
maendeleo ya mkoa wa Lindi iliyowasilishwa kwake na Mkuu wa mkoa huo,
Godfrey Zambi.
“Mkuu wa Magereza wa mkoa atembee
gereza ambalo wanashikiliwa watuhumiwa wa dawa za kulevya na aangalie
mradi unaolenga kupeleka maji gerezani hapo kama ni kweli au njia…,”
amesema Waziri Mkuu, Majaliwa.
Aidha, Waziri Mkuu, Majaliwa
amemtaka mkuu huyo wa Magereza kujiridhisha kama ulinzi na usalama wao
umeimarishwa na kuhakikisha hakuna mtuhumiwa anayetoweka.
Awali akisoma taarifa kwa Waziri
Mkuu, mkuu wa mkoa wa Lindi, Zambi amesema matumizi ya dawa za kulevya
hususan kwa vijana ni miongoni mwa changamoto zinazoukabili mkoa huu
ambapo wilaya ya Kilwa inaongoza kwa kuwa na waathirika wengi.
Amesema matumizi ya dawa hizo
yanasababisha kupunguza kwa nguvu kazi kwani watumiaji wengi ni vijana,
hivyo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali katika kupiga
vita matumizi ya dawa hizo kwa kuwafichua wauzaji na watumiaji.






0 maoni:
Chapisha Maoni