Jumatatu, 16 Mei 2016

WANANCHI KITONGA WAANDAMANA KUPINGA UFUNGWAJI WA HOTELIHOTEL YA STARCOM


WANANCHI  wa kijiji cha Mahenge wilaya ya Kilolo mkoani Iringa  wailalamikia Halmashauri ya wilaya ya Kilolo kwa kuifunga hoteli ya Star Com kuwakosesha ajira zaidi ya watu 2500 waliokuwa wakinufaika na Hoteli 
Kutokana na uamuzi wa Halmashauri ya Kilolo kuifunga Hoteli hiyo,wananchi hao wamepanga kuandamana kwenda kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo ama mkuu wa mkoa wa Iringa kudai haki yao .
Wakizungumza na wandishi wa habari jana  wananchi hai walisema kufungwa kwa hoteli hiyo kwa zaidi ya wiki mbili sasa,
kumechangia wakulima ambao walikuwa wakiuza mazao yao kukosa soko pia wafanyakazi kuendelea kuishi katika mazingira ya shida.
 “Ni ukweli usiopingika kuwa   hoteli hii inapigwa vita ya kibiashara na
 baadhi ya washindani wenzake wanaofanya biashara ya huduma
za vyakula kwa abiria wanaosafiri katika ya Dar es Salaam na
mikoa ya kusini hilo hakuna asiyejua hata baadhi ya madiwani na viongozi wa Halmashauri wanahusika"alisema Shukran Mgao 
“mimi pamoja na wenzangu ni wajasiriamali
tuliokuwa tunauza nyanya na vitunguu hotelini hapa na kwa
abiria wa mabasi yanayosimama hapa. Sielewi kwa uamuzi huu
wanataka akina mama na vijana wengine wanaoitegemea kupata
vipato, wafanye ninini.”
 Bw. Maulid Mbugi alisema maamuzi hayo yamewakasirisha
wananchi wengi wa kijiji hicho hatua inayowalazimu
kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya kupeleka kilio chao.
“Hatutaki vijana wanaoitegemea hoteli hii wajiingize
kwenye vitendo vya ujambazi na akina dada wajiingize kwenye
vitendo vya ngono...
 Tunaomba serikali ifungue hoteli hii
kwasababu dosari zinazotajwa zinaweza kurekebishwa wakati
ikiendelea kutoa huduma,” alisema.
Meneja wa hoteli hiyo, Michael George alisema; “mbali na
kuwaathiri wananchi walio jirani nayo, kufungwa kwa hoteli
 hiyo kumewaathiri pia wafanyakazi wa hoteli hiyo na familia
zao.”
Akizungumzia uamuzi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuifunga
hoteli hiyo, Mkurugenzi wa hoteli hiyo, Henry Vegula 
“tuliopokea kwa mikono mwili pamoja na kwamba
marekebisho yanayotajwa tungeweza kuyafanya wakati tukitoa
huduma ili wananchi, wafanyakazi na wateja wetu
wasiathirike.”
Alisema pamoja na uamuzi wake, tayari uongozi wa hoteli hiyo
umekwishafanya marekebisho mbalimbali muhimu kama
ilivyoelekezwa na halmashauri hiyo na akaomba serikali
iwafungulie ili waendelee kutoa huduma.
Kwa mujibu wa barua ya Afisa Afya wa Wilaya ya Kilolo,
Fanuel Nyadwike, hoteli hiyo imefungwa baada ya timu ya
idara ya afya ya halmashauri hiyo kufanya ukaguzi Machi 22,
mwaka huu na kunaini ikiwa na mapungu mbalimbali.
Mapungufu hayo kwa mujibu wa barua hiyo yenye  Kumb Na.
KDC/H2/11/16 ni pamoja na uchakavu wa sakafu, kuta, paa na
mitaro ya maji katika eneo la jiko.
Mengine ni masinki ya choo, vigae katika meza za jikono na
eneo la utekeketezaji taka ngumu ambalo awali lilikuwa
limejaa na halifai kuendelea kutumika.
 Katika kuiboresha zaidi hoteli hiyo, Vegula alisema mipango
 yao ni pamoja na kuboresha mfumo mzima wa maji taka kwa
 kuzingatia kanuni na sheria za mazingira.

0 maoni:

Chapisha Maoni