Jumatatu, 23 Oktoba 2017

WANAFUNZI WAMETAKIWA KUJIEPUSHA NA MAMBO YANAYOWEZA KUKATIZA NDOTO ZAO

Posted by Esta Malibiche On Oct 23,2017 In NEWS

Mkuu wa Shule ya Sekondari Lyang'a  inayomilikiwa na kanisa katoliki parokia ya Mtakatifu Yoseph Itengule jimbo katoliki la Iringa, Padre Renatus Shija akizungumza katika mahafali ya 3 ya shule hiyo yaliyofanyika jana huku yakiambatana na harambee ya kuchangia ununuzi wa garei la Shule.PICHA NA ESTA AMALIBICHE.

Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini Anthony Komu aliye katikakati,akiongoza harambee ya kuchangia ununuzi wa gari la shule katika mahafali ya 3 ya shule ya sekondari Lyang'a,kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa dadi Igogo na kulia kawake ni Mkuu wa Shule hiyo Padre Renatus Shija.

Marcelina Mkini,ambae ni Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo akizungumza katika mahafali ya 3 ya shule ya Sekondari Lyang'a yaliyofanyika jana.
Grace Moshi mhitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Lyang'a akisoma Risala ya wahitimu.





Na Esta Malibiche.
WANAFUNZI nchini wametakiwa kuutumia muda wao mwingi katika masomo ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii  ili Taifa liweze kuwa na viongozi bora wenye kulileta mabadiliko chanya.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mbunge wa jimbo la Moshi Mjini,Anthony Komu wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Lyang”a  kwenye mahafali ya tau tangu kuanzishwa kwa shule  inayomilikiwa na kanisa katoliki Parokia ya Mtakatifu Yoseph Itengule iliyopo katika kijiji cha Itengule,kata ya Malangali,Halmashauri ya Mufindi Mkoani Iringa .

Kimu alisema kuwa Moja ya changamoto kubwa   tuliyonayo watanzania ni ukosefu wa Elimu bora,na ili Taifa liweze kusonga mbele kimaendeleo linahitaji viongozi wenye Elimu,hivyo ninawaomba mzingatie yale mliyofundishwa  na walimu ili muweze kufanya vizuri katika mitihani yenu mnayotarajia kuanza hivi punde’’’Alisema Kimu.

Aidha  aliwasihi wahitimu mara wamalizapo mitihani wawe watulivu  wakati wanasubiri matokeo ,na hatimae kuendelea na masomo ya kidato cha tano.

‘’Ninawaomba mkirudi nyumbani kwa muda huu mfupi wa kusubiri matokea,zinmgatieni maadili  mliyofundishwa mkiwa hapa shuleni,bado nyie ni wanafunzi hakikisheni  mnajiepusha na mambo yasiyofaa ambayo yanaweza kukatisha ndoto zenu za kuendelea na masomno ya juu.’’’Alisema Kimu’

Awali Mkuu wa Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa katoliki parokia ya Mtakatifu Yoseph Itengule jimbo katoliki la Iringa, akimkaribisha Mgeni rasmi,Padre Renatus Shija lisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na chanvgamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la gari la shule ambalo lingeweza kuwasaidia  katika utoaji wa   huduma za Afya,na usafiri pindi shule inapokuwa imefunga kwa wanafunzi na wafanyakazi kwa ujumla.

Padre Shija alisema kuwa pamoja na changamoto hiyo,laikini wameweza kufanikiwa kujenga maabala  ya kisasa mbayo ni kwaajili ya masomo ya Fizikia,Biolojia,Kemia na Jigrafia,Wamejenga maktaba kwa ajili ya wanafunzi kujisomea ili kujiongezea ujuzi na maarifa zaidi.

‘’T umepunguza  tatizo la maji kwa kuchimba kisima chenye urefu wa mita 120, na tumeanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa ambao umesaidia wanafunzi kujisomea hadi usiku ukilinganisha na hapo awali ambapo tulikuwa tunatumia umeme wa jua[Solar]pia umesaidia kuratibu kazi mbalimbali za shule’’Alisema Padre Shija 

Alisema kuwa wamefanikiwa kuongeza walimu kutoka 17 hadi kufikia walimu 21 na wafanyakazi wasiuo walimu kutoka 7 na kufikia 11,pamoja na kuanzisha kidato cha tano na sita kwa michepuo ya sayansi na sanaa.Pia wamefanikiwa  kuboresha viwanja  vya michezo wa mpira wa miguu,pete na mpira vwa wavu,kupanda  kitaaluma,hii imetokana  na  matokeo ya kidato cha nne 2015 ambapo wanafunzi wawili walipata daraja la nne na mwaka 2016 kufuta kabisa daraja la nne.Pia wameongeza mabweni ya kulala wavulana na wasichana.

Akizungumzia matarajio ya shule hiyo,alisema kuwa wanatarajia  kuongeza majengo ya shule ikiwemo madarasa,jingo la utawala na maktaba ya kisasa,kuongeza michepuo ya masomo kwa kidato cha tano na sita kwa masomo  ya Sayansi.

Grace Moshi akisoma Risala ya Wahitimu wa kidato cha nne alisema kuwa   shule hiyo iliyoanzishwa mwa 2012 imeweza kuwalea wanafunzi katika taaluma,madili mema,nidhamu safi na sala,hivyo kuwa mfano kwa shule  zingine na jamii kwa ujumla.

‘’Ndugu Mgeni rasmi  tunapenda kutoa shukrani zetu kwa  kwa bodi ya Shule,uongozi wa shule,Walimu,Wafanyakazi wotekatika idara mbalimbali,Polisi Malangali,Wankiji cha Utengule,wazazi na walezi wetu ambao kwa moyo wao wamejitolea kutulea na kuhakikisha tunafanikisha kuupata Elimu tuliyonayo leo’’’alisema..

Alisema shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa nyumba za walimu na wafanyakazi, hali inayopelekea  walimu kukaa mbali na shule hivyo kushindwa kutoa huduma kwa wakati.Pia shule inakabiliwa na  upungufu wa maji kutokana na kisima kilichopo hakikidhi mahitaji ya wanafunzi kutokana na uwingi wao.

Mahafari hayo yaliambatana na harambee ya kuchangia ununuzi wa gari la Shule,ambapo jumla ya kiasi cha Tsh.9.2 Mill. zilichangwa huku mgeni rasimi akichanga kiasi cha Tsh. 2.Mill. Pia jumla ya wahitimu 49,walitunukiwa vyeti.

0 maoni:

Chapisha Maoni