Katika siku za hivi karibuni
katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kumejitokeza makundi ya watu ama
mtu binafsi kutumia mwamvuri wa taasisi fulani kujipatia kipato kwa njia
za udanganyifu (utapeli) kwa kuwaahidi vijana kwamba watawapatia ajira
katika taasisi hizo.
Makundi haya ya kihalifu
imebainika kwamba yapo katika maeneo mbalimbali, hivyo, ni suala ambalo
linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ili kukomesha vitendo
hivyo. Juhudi za makusudi zinaendelea kufanyika na jeshi la polisi ili
kuwatia mbaroni watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kitapeli.
Aidha, kufuatia kuibuka kwa
vitendo hivyo, tayari Jeshi la Polisi limewakamata matapeli wawili
wakiwa wamekusanya vijana katika mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya,
uchunguzi dhidi yao unaendelea na pindi utakapokamilika watafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabiri.
Jeshi la Polisi likishirikiana na
vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, kimsingi, kazi yetu kubwa ni
kuhakikisha Tanzania inakuwa na Ulinzi na Usalama imara. Tutaendelea
kupambana na makundi haya ya kihalifu na utapeli ili nchi yetu iendelee
kuwa salama.
Tunawasihi wananchi kufuatilia
taarifa kwenye vyanzo sahihi juu ya jambo lolote wanalotaka kulifanya
ili kuepuka utapeli unaoweza kufanywa na baadhi ya watu kwa lengo la
kujipatia vipato. Aidha, wananchi watoe taarifa kwenye vyombo vya
usalama kuhusu tabia na mienendo yoyote wanayoitilia mashaka. Jeshi la
Polisi na vyombo vingine vyote vya Ulinzi na Usalama viko imara,
makundi ya kiuhalifu na wahalifu wote wajue hawana pa kukimbilia,
watakamatwa.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
0 maoni:
Chapisha Maoni