Kiongozi
wa mashtaka nchini Argentina ameomba idhini ya mahakama kuanzisha
uchunguzi katika shughuli za aliyekuwa rais wa taifa hilo, Cristina
Fernandes de Kirchner, juu ya madai kuwa alishiriki katika utakasaji wa
pesa haramu.
Uamuzi
huo unafuatia ushahidi uliotolewa mahakama Ijumaa na mfanya biashara,
Leonardo Farina mshirika wake yeye na mumewe ambaye pia alikuwa ni rais
wa Argentina bwanaNestor Kirchner .
Akitoa
ushahidi baada ya kuahidiwa kusamehewa makosa yake mfanyabiashara huyo
alisema kuwa Bi Fernandez na marehemu mumewe Nestor Kirchner walishiriki
katika shughuli kadhaa ya ulaghai wa fedha za umma.
Image copyrightGettyImage captionUchunguzi huo unatokana na ufichuzi uliotokea kwenye kampuni ya Mossack Fonseca
Mfanyabiashara
mwingine ambaye pia ni mwandani wa familia ya Kirchner, Lazare Baez,
alitiwa mbaroni mapema juma lililopita na kulaumiwa kwa ulaghai wa Dola
Milioni tano
0 maoni:
Chapisha Maoni