Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi Mhe. William Ole Nasha (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kikazi
Gereza Kwamugumi, Korogwe Mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi
iliyotolewa na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John
Casmir Minja inaeleza kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea
maendeleo ya mradi wa mabwawa ya samaki yaliyopo gerezani hapo ambayo
hadi sasa yamepandwa vifaranga wa samaki 18,800 tangu tarehe 16/12/2015.
Kabla ya kutembelea eneo la mradi
wa mabwawa ya samaki, Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha atapokea taarifa
fupi ya maendeleo ya mradi wa uzalishaji samaki Gereza Kwamugumi,
Korogwe.
Miradi ya ufugaji samaki ipo
katika Magereza ya Karanga, Njombe, Masasi, Tukuyu ambapo nia ya Uongozi
wa Jeshi la Magereza ni kuieneza katika Magereza mbalimbali yenye fursa
za kuendesha mradi huo.
Mradi wa uzalishaji samaki katika
Gereza Kwamugumi ni mojawapo ya miradi mbalimbali ya uzalishaji mali
iliyoanzishwa na Uongozi wa Jeshi katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali zinazolikabili Jeshi la Magereza, hususan katika kuipunguzia
Serikali gharama za kuhudumia Magereza na kuongeza pato la kodi kwa
Taifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni