Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla (wa
pili kushoto) akisikiliza kwa makini mazungumzo na Afisa miradi
anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa
wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile (wa kwanza kulia). Wengine
ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayeshughulikia magonjwa yasiyo
ambukiza, Profesa Ayoub Magimba (katikati), akifutiwa na Mkurugenzi
taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaisalage na kushoto Mratibu wa
Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwa watu
wazima, Dk. Sara Maongezi. (Picha na mpiga picha wetu).
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla
amekutana na Afisa miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika
kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon
Haile katika mazungumzo yaliyofanyika leo asubuhi Aprili 14.2016,
Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Dk.
Kigwangalla ameomba Tanzania ipatiwe kibali cha kununua mashine mpya ya
kutibu saratani (LINAC) Sambamba na sehemu ya msaada iliyoahidiwa na
Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Bw.Yukiko Amano mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu,
Mh. Mizengo Kayanda Pinda miaka mitatu iliyopita.
Tanzania tayari imetenga kiasi
cha Euro 1.65 Milioni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mchango wake kwa
asilimia 50 kama mradi ulivyokuwa awali.
Mh. Kigwangalla alisema:
“Bahati mbaya sana kutokana na ucheleweshwaji, Bajeti ya msaada huo
kutoka IAEA ilipitwa na wakati na kusababisha Tanzania kukosa fursa
hiyo. Malengo ya Tanzania ni kununua mashine hizo mbili kwa ajili ya
kuboresha huduma za tiba ya Mionzi nchini”.
Ujenzi wa jengo kwa ajili ya
kufunga mashine hizo mbili umesha kamilika na mashine moja itakamilika
mwaka huu na ya pili mwakani ili kuboresha huduma za Saratani nchini.
Katika mazungumzo hayo, Maafisa
waandamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Woto
walishiriki, akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba
anayeshughulikia magonjwa yasiyo ambukiza, Profesa Ayoub Magimba,
Mratibu wa Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa
yasiyoambukiza kwa watu wazima, Dk. Sara Maongezi pamoja na Kaimu
Mkurugenzi taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage.
0 maoni:
Chapisha Maoni