(Picha zote na Mpigapicha Wetu).
……………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu,
TAASISI
ya kidini ya Memon Jamaat imekabidhi msaada wa madawati 160, Printer
pamoja kuweka mfumo wa umeme (wiring) katika Shule ya Sekondari
Mikocheni, Dar es Salaam vikiwa na thamani ya shilingi milioni 22.3.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Yusuf Esack
Ayub alisema msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali
za kuboresha sekta ya elimu kupitia mpango wake wa elimu bure.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa licha ya Serikali kuanzisha mpango wa elimu bure
nchini haiwazuii wao kama wadau wa elimu kusaidia maendeleo ya elimu
nchini na hivyo kuamua kuisaidia shule hiyo pekee ya Serikali ya
Sekondari katika Kata ya Mikocheni ili iweze kuleta ushindani mkubwa wa
kielimu.
“Sisi
tumeitikia ilani ya Rais wetu John Magufuli ya elimu bure na kuamua
kuleta msada huu utakaokuwa endelevu shuleni hapa. Pia tutafanya mpango
wa kuleta vifaa vya maabara ili tupate wataalamu wazuri kutoka shule
hii.” Alisema Mwenyekiti uhuyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo na Meya Mstaafu wa Manispaa
ya Kinondoni, Yusuph Mwenda aliwashukuru wafadhili hao na kuomba wadau
wengine wa elimu kujitokeza kuisaidia shule hiyo katika maeneo mengine
ya kielimu.
Mwenda
alisema kuwa misaada kama hiyo sit u inasaidia maendeleo ya shule ila
inasaidia pia hata familia za hali ya chini ambazo ndizo zenye watoto
wanaosoma katika shule hizo na kusisitiza kuwa wadau wa elimu wana
wajibu wa kuunga mkono kauli ya Rais John Magufuli ya elimu bure kwa
kusaidia maeneo mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule.
“Tunashukuru
Memon Jamaat kwa moyo wenu mliokuwa nao wa kuja kuisaidia shule hii.
Mnachokifanya nyie kwanza mnawasaidia watoto wa kitanzania, hizi shule
za Kata wanaosoma ni watoto wa watu wa kawaida sana, huwezi kwenda
kuwasaidia kwenye nyumba zao, ukisaidia kuboresha mazingira ya elimu
unawasaidia wao na familia zao, lakini unaisaidia nchi itakuja kupata
wataalamu wazuri watakaokuja kuisaidia Tanzania, mi nawashukuru sana.”
Alisema Yusuph Mwenda.
Mwenyekiti
huyo alizitaka taasisi nyingine kujitokeza kusaidia shule hiyo pamoja
na nyingine za Serikali ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Srikali ya
Rais John Magufuli za kuboresha sekta ya elimu nchini.
Naye
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Salama Ndiyetabura alisema kuwa baada ya
kuwekewa mifumo ya umeme na taasisi hiyo, walifanya mawasiliano na
Tanesco na kuwaahidi kuleta mkaguzi wao na kuwaingizia umeme mara moja.






0 maoni:
Chapisha Maoni