Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma
Kaskazini akisisitiza jambo mbele ya vijana wa Kitanzania waishio New
York. Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana hao waliotaka kujua
maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya bunge la jamhuri
anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi kupitia upinzani, pia
yeye kama mwana siasa alie upande wa upinzani nini mtazamo wake juu ya
kasi ya rais wa wamu ya 5. Zitto ni mmoja ya vijana kwenye Bunge la
jamhuri ya muungano wa Tanzania na ni Mbunge mwenye nguvu na uwezo wa
kuwakirisha hoja zenye mashiko ndani ya bunge la jamhuri na kuitikisa
serikali ya chama tawala. Mfano mmoja ni suala la Escrow yeye ndiyo
alikuwa chanzo cha habari hiyo iliyotikisa serikali na kupelekea
wananchi kukosa imani na mwenendo mzima wa serikali ya chama tawala. Na
pia alisha wasilisha hoja ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa
ubunge kwa miezi 4. Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank
na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University New York na
kuongea na wasomi wa huko na pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard
University huko Boston. MA. Picha na Vijimambo Blog New York
0 maoni:
Chapisha Maoni