Ijumaa, 15 Aprili 2016

(TUMA) KIMELITAKA BARAZA LA SANAA LA TANZANIA KUTOFUNGIA MATAMASHA YA WASANII BILA KUSHIRIKISHWA

1Katibu Mkuu wa CHAMA cha Muziki wa kizazi kipya Tanzania Urban Music Association (TUMA), Samweli Andrew Mbwana maarufu kama Briton (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam juu ya uundaji wa kamati na viongozi wa kamati ndani ya chama hicho, kushoto ni Afisa uhusino wa Chama hicho, Bagdad Kweka.
2Katibu Mkuu wa TUMA, Samweli Andrew Mbwana maarufu kama Briton (kulia) akionesha baadhi ya kadi za wanachama waliojiunga na chama cha wasanii TUMA,kushoto ni Afisa Uhusino wa Chama hicho, Bagdad Kweka.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
…………………………………………………………………………………………
CHAMA cha Muziki wa kizazi kipya Tanzania Urban Music Association (TUMA) kimelitaka Baraza la Sanaa la Tanzania kutofungia musiki  au matamasha ya wasanii bila kushirikisha chama hicho.
Katibu Mkuu wa TUMA Samweli Andrew Mbwana maarufu kama Briton ameyasema hayo wakati alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia uundaji wa kamati na viongozi wa kamati hizo ndani ya chama.
“Kutokana na ukuaji wa teknolojia na maendeleo ya kimusik ni lazima wasanii nao wabadiliki ili kuendana na soko la kimataifa ila kufungia musiki wa msanii wakati nyimbo nyingine kama hiyo inaendela kuchezwa ni kwenye vituo vya radio ni kurudish nyuma maendeleo ya musiki” alisema.
Aidha ilitaja kamati hizo kuwa ni kamati ya nidhamu na madili ni burudani na matukio, mipango, fedha na uchumi, habari na mawasiliano, ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.
“Wito kwa wasanii wote wa muziki wa kizazi kipya kutii maagizo ya serekali kwa kufannya kazi kwa kufuata utaratibu, sheria na kanuni, kusajili kazi za na kujisajili kwenye chama hicho” Alisema

0 maoni:

Chapisha Maoni