Na Bashir Nkoromo, Njombe
………………………………………………
Watumishi
wa Chama ni sehemu muhimu inayokifanya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuendelea kuwa bora na imara kwa kuwa ndiyo jiko la kubuni na kuandaa
taswira ya muonekano wa Chama katika jamii.
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajabu Luhwavi wakati
akizungumza na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi kutoka wilaya za mkoa wa
Njombe na Ruvuma, jana, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo
kuzungumza na kusikiliza changamoto na kero zinazowakabili watumishi wa
Chama.
Alisema,
ni kutokana na kutambua umuhimu wa watumishi hao ndiyo sababu Chama Cha
Mapinduzi kinafanya kila jitihada kuhakikisha kinakutana nao ili kujua
mazigira walioyomo na changamoto na kero zinazowakabili ili kuweza
kutafuta njia za kuzitatua kwa kadri inavyowezekana.
“Unajua
mimi ndiyo nasimamia utumishi katika chama, kazi zingine zote
zinazonihusu naweza kuzifanya kupitia mafaili nikiwa ofisini, lakini
hili la kuhusu mazingira na hali za watumishi ambalo pia linanihusu
siweze kulifanya nikiwa ofisini, ndiyo sababu nimeamua kufanya ziara
hizi, ili niwasilikilize kero na changamoto zinazowakabili tukiwa
pamoja”, alisema Luhwavi.
0 maoni:
Chapisha Maoni