Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
……………………………………………………………………………………..
Na John Stephen
Kamati
ya Afya ya Bunge leo imeitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
kwa ajili ya kukagua huduma mbalimbali za afya zinazotolewa na
hospitali hiyo.
Ziara
hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Joseph Serukamba
akiwamo Mussa Azzan Zungu na wabunge wengine wa kamati hiyo.
Wabunge
hao wametembelea Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Idara ya
Magonjwa ya Akili, Idara ya Mionzi na Wodi ya Mwaisela na chumba cha
kuchakacha gesi ambayo inatumika wakati wa kutoa tiba kwa wagonjwa
mbalimbali.
Daktari
wa magonjwa ya Dharura na Ajali, Upendo Ndara amewaeleza wabunge hao
jinsi madaktari na wauguzi wanavyowahudumia wagonjwa wanaofikishwa
kwenye idara hiyo, changamoto na jinsi wanavyofanikiwa kuokoa maisha ya
wagonjwa wa ajali na wagonjwa wengine.
Pia,
Dk Upendo ameelezea juhudi kubwa zinazofanywa na Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) katika kupanua jengo la idara hiyo ili kutoa huduma bora
za matibabu kwa wagonjwa.
Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Frank Massawe amewaeleza wabunge mafanikio yaliopatikana baada ya wagonjwa wa akili kupatiwa matibabu na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.
Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Frank Massawe amewaeleza wabunge mafanikio yaliopatikana baada ya wagonjwa wa akili kupatiwa matibabu na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.






0 maoni:
Chapisha Maoni