Alshabab wavamia kituo cha polisi Wajir Kenya
Wapiganaji takriban 100 wa kundi la kigaidi la Alshabab wamevamia kituo kimoja cha polisi Wajir Kaskazini mwa Kenya.
''wavamizi walishambulia kituo cha polisi cha Diff na wakakabiliwa vikali na askari waliokuwepo, wengi wao walijeruhiwa ila walifaulu kuteka nyara gari la serikali la kituo cha Diff ambalo walitumia kuwabeba majeruhi wao'' alisema Inspekta Jenerali wa polisi wa Kenya Joseph Boinnet.
Maafisa 3 wa polisi wa Kenya walijeruhiwa.
Kundi hilo lilitorokea mpakani.
Kikosi cha jeshi la Kenya limewafuata huko baada yao kuvuka mpaka kati ya Kenya na Somalia.






0 maoni:
Chapisha Maoni