AFISA Elimu
Msingi Manispaa ya Iringaa Haji Mnasi
ameungana na walimu wake kuingia
darasani na kufundisha ikiwa ni
utekelezaji wa mataala kwa vitendo.
Akizungumza
na mtandao huu wa kali ya habari leo hii katika ofisi kwake alisema kuwa ameamua kufundisha ili kuwatia moyo walimu
wake katika zoezi la ufundishwaji.
Mnasi
alisema akiwa Afisa Elimu pia kitaaluma
ni mwalimu,hivyo katika uataratibu alioupanga kwa kushirikiana na walimu katika
viakao vya kazi atahakikisha anaingia darasani katika shule tofauti zilizopo
ndani ya manispaa yake ili kuwaongezea maalifa wanafunzi ambayo wanapewa na walimu wao
Miongoni mwa
shule alizoingia na kufundisha nipamoja na shule ya Msingi Shule ambazo
ameingia na Sabasaba,Njiapanda,Mlangali,Maendeleo ,Azimio pamoja na shule ya
Msingi Kihesa hizi zote zipo ndani ya manispaa yake.
‘’’’’Mimi ni
mwalimu kitaaluma,hivyo sina budi kushirikina na walimu wangu kuifundisha ili kuendana na kasi yam h. rais wetu dkt
John Pombe Magufuli kwa kutokukaa ofisini siku zote na kuzungusha kiti bila
kuzunguka katika maeneo ya shule zangu na kuangalia changamoto zinazowakabili
walimu na wanafunzi ‘’aliasema mmas
Aidha Afisa
Elimu alisema katika Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa inajumala ya shule za msingi 50 zikiwemo shule za serikali 43,zenye wanafunzi 25133
wakiwemo wavulan 12352 na wasishana
12781 na kwa shule zisizo za serikali
ziko 7,idadi ya wanafunzi wako 3347,wakiwemo wavulanan 1622 na wasichana 1725.
Alisema jumla ya walimu katika shule za
serikali wako 778 wakiwemo wanaume 150,na wanawake628 ,na kwa shule zisizo za serikali zina walimu 129 wakiwemo
wanaume 62,na wanawake67.
Alisema tangu
Mh. Rais atangaze Elimu bila malipo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imepokea
kiasi cha Tsh.69,049,00/ kwa awamu ya tatu
yaani Desembailipokea jumla ya
23,954,000,Januari ilipokea jumla 23,115,000 na Februari ilipokea jumla ya
kiasi cha Tsh.21,980,000,hizi zote zimetumika kama ilivyopangwa.
‘’’’Pamoja
na mafanikio hayo,katika shuguli za utekelezaji wa utoaji Elimu tumekuwa tukikabiliwa na chanamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya
baadhi ya shule ambazo zina umri mkubwa,msongamano wa wa watoto hasa kwa
madarasa ya awali na la kwanza kama matokeo ya Elimu bure na kupelekea upungufu
wa madarasa,madawati na vyoo, pamoja na ufinyu wa bajeti kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu hususani ya majiko na mahali pa chakula kwa wanafunzi’’’alisema
‘’’’’’Tumepanga
mikakati kuakabiliana na changamoto hizo ambayo ni kuhakikisha tunatengeneza
madawati mapya 2,803 kwa sasa madawati 1150 ytayari yanatengenezwa,kukarabati
madwati yaliyochakaa,kuitisha harambee itakayoshirikisha wadau mbalimbali ili
kuchangia madawati na ujenzi wa wa
nvyumba vya madarasa pamoja na kutafuta wafadhiri ndani na nje ya manispaa ya
Iringa’’’’alisema






0 maoni:
Chapisha Maoni