Posted by Esta Malibiche on Sept6.2016 in Teknolojia with No Comment
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya shughuli za utafiti
na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa
kampuni ya Dorsal Bw,P.K Surendran na wa pili kushoto kwake ni
Mkurugenzi Mtendaji Heritage Rukwa Tanzania Limited.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya
Dorsal Bw,P.K Surendran akizungumza kuhusu hatua iliyofikiwa ya shughuli
za utafutaji wa mafuta na Gesi.Kushoto kwa Mkurugenzi uyo ni Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mtendaji
Heritage Rukwa Tanzania Limited Bw Jim Baban(wa tatu kushoto),Meneja
Mkazi wa shirika la Statoil Tanzania фystein Michelsen na Kaimu
kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petrol nchini Bw.James Andilile.
Wadau wa Gesi na Mafuta
wakimskiliza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
(hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya shughuli za
utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw.Kapulya Msomba akieleza
maendeleo ya shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi
yaliyofikiwa na shirika hilo kwa wadau wa Mafuta na Gesi jijini Dar es
Salaam.Kushoto kwake ni Kaimu kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petrol
nchini Bw.James Andilile na Meneja Mkazi wa shirika la Statoil
Tanzania Bw. фystein Michelsen.
Kaimu kamishna wa Nishati na
Maendeleo ya Petroli nchini Bw.James Andilile akijadili na wadau wa
mafuta na gesi shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi
nchini.Kushoto kwake Meneja Mkazi wa shirika la Statoil Tanzania
фystein Michelsen.
Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya
Heritage Rukwa Tanzania Limited Bw Jim Baban akichangia jambo wakati wa
kikao cha kujadili maendeleo ya shughuli za utafiti na uchimbaji wa
mafuta na gesi nchini.Kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Dorsal Bw,P.K
Surendran.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
0 maoni:
Chapisha Maoni