Posted by Esta Malibicheon Sept3.2016
in
KITAIFA
|
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi(kulia) akimsikisiliza Meneja wa TRA, Mkoa wa Kikodi Kinondoni Wallace Mnkande alipofanya ziara katika ofisi za TRA Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam. |
Na: Frank Shija & Sheila Simba
Walipa
Kodi nchini wametakiwa kulipa Kodi kwa wakati na kwa kiwango
kinachostahili kulipwa kwa ni Serikali inatoa huduma za kijamii kutokana
na kodi hizo.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi
alipotembelea Ofisi za Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi wa
Kinondoni leo Jijini Dar es Salaam.
Hapi
amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais, Magufuli katika
vipaumbele vyake ni pamoja na kuhakikisha watu wanaostahili kulipa Kodi
wanalipa kwa wakati kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Aliongeza kuwa ili Serikali kutimiza haki ya utoaji wa huduma za msingi ni lazima watu walipe Kodi.
“
TRA hakikisheni kila anayestahili kulipa Kodi analipa kwa wakati na
kiwango stahiki, kwani Serikali inaendeshwa kwa Kodi, Elimu bure,huduma
za Afya , maji na mengine chanzo ni kodi” Alisema Hapi.
Serikali
itatoa ushirikiano wowote utakaohitaji ili kusaidi udhibiti wa wakwepa
kodi kupitia vyombo vya dola na mamlaka zingine ili kusafikisha azma ya
kila anayestahili kulipa kodi alipe kwa wakati bila kujali ni nani.
Aidha
alitoa ushuri kwa uongozi wa Mamlaka hiyo kuboresha mfumo wa utoaji wa
huduma kwa wateja wao ili kuondoa malalamiko yasiyo ya msingi.
Kwa
upande wake Meneja wa TRA, Mkoa wa Kikodi wa Kinondoni, Wallace Mnkande
amesema kuwa wamevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya
shilingi bilioni 3 ambapo jumla ya shilingi bilioni 43 zimekusanywa kwa
mwezi Agosti huku lengo likiwa ni shilingi bilioni 40.57.
Meneja
huyo ameongeza kuwa TRA Kinondoni wamejipanga kuhakikisha wanaongeza
ukusanyaji wa Kodi ili kuvuka malengo zaidi kwani ni eneo ambalo
linawalipa kodi wengi na wakubwa.
Katika
kurahisisha utendaji wa majukumu TRA Kinondoni imegawa ofisi zake
katika kanda nne ambazo ni Tegeta, Manzese, Kimara na Millenium Tower
kwa ajili ya walipa kodi za Leseni za Madereva.
0 maoni:
Chapisha Maoni