Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh.Mrisho Gambo akihutubia wageni katika hafla hiyo |
Meza Kuu ambapo wageni rasmi waliketi katika hafla hiyo |
Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera akizungumza wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo |
Kutoka kushoto ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha Mjini Mh.Felix Mrema, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko BRITAM Kenya na mwisho ni Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera |
Meneja BRITAM Tanzania tawi la Arusha Bi. Loisi Yatera akiwatambulisha baadhi ya watendaji wa Kampuni hiyo mbele ya wageni waliohudhuria katika hafla hiyo |
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo katika hoteli ya Mount Meru |
Mbunge wa Arusha Mjini Mh.Godbless Lema pamoja na mke wake wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika hafla hiyo ndani ya Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha |
Mkurugenzi BRITAM Kenya Bw.Stephen Wandera akimsikiliza kwa makini mgeni rasmi wakati akihutubia wageni katika hafla hiyo |
Habari na Woinde Shizza,Arusha.
Kampuni
ya Bima ya Britam imeadhimisha miaka 50 ya kutoa huduma za bima nchini
Tanzania huku ikiongoza katika utoaji wa huduma bora za bima za
magari,nyumba ,mali pamoja na afya.
Sherehe
za Maadhimisho hayo zimefanyika katika Hotel ya Mount Meru iliyoko
jijini Arusha na kuudhuriwa na Viongozi wa kiserikali pamoja na Wadau wa
Bima.
Afisa
Mkuu wa Kampuni hiyo nchini Tanzania Stephen Lokonyo amesema kuwa
kampuni hiyo imejipanga vizuri kuwahudumia watanzania na kuwafikia watu
wengi zaidi ili waweze kunufaika na huduma za bima .
Aliongeza
kuwa wao kama kampuni ya bima ya Britam wamejipanga kuwasaidia wananchi
mbalimbali wakiwemo wa juu pamoja na wachini kwakuanzisha bima za aina
mbalimbali ikiwemo ya mali zao kama nyumba ,bima za afya pamoja bima ya
kilimo kwa ajili ya wakulima pamoja na wafugaji.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliwataka mashirika ya bima
kuwafikiria pia madereva bodaboda kwa kuwaanzishia bima za afya pamoja
na bima za vyombo vyao ili pale wanapopata matatizo kama ya kuunguliwa
na piki piki zao pamoja na kupata ajali waweze kusaidika kwa uraisi matibabu na kufidiwa pindi wanapopata ajali.
Alisema
kuwa kumekuwa na pikipiki nyingi sana hivyo iwapo wataanzisha bima kwa
ajili ya pikipiki wataweza kuwasaidia sana vijana pia wataweza kupata
wateja wengi waotumia vyombo hivi.
0 maoni:
Chapisha Maoni